Connect with us

Video | Audio: Gift Mwamba – Uvumilivu

Audio

Video | Audio: Gift Mwamba – Uvumilivu

Baada ya kimya cha muda wa takribani miaka miwili toka alipoachia nyimbo zake kama vile Ndoa na Uwepo wa Mungu mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Gift Mwamba kutoka jiji Dar es salaam kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia video ya wimbo wake mzuri uitwao Uvumilivu.

Video ya wimbo huu imeongozwa na director Nosa kutoka studio za Nosa Pictures Production na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za Sharom, chini ya producer Eddo Montana.

“Japo matatizo ni mengi ila usiyape nafasi, Imani yako ndio nguzo majaribu yafanye kuwa mtaji simama katika Imani kwakuwa chini ya jua hakuna lililogumu mwamini yeye ukimwomba yote yanawezekana. Uvumilivu ni neno dogo sana ila ndio kila kitu katika maisha yetu, chochote unachokifanya kinahitaji uvumilivu, Nakukaribisha sasa kutazama video hii na nina imani kuwa hutabaki kama ulivyo, UVUMILIVU NI MTAJI ATAKUTAJIRISHA MUNGU TU.” – alisema Gift Mwamba

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Gift Mwamba amesema kuwa anamshukuru Mungu sana kwakuwa sasa amekamilisha albamu yenye nyimbo 8 inayobebwa kwa jina la Uvumilivu ikiwa ni wimbo aliouachia pamoja na video.pia nipo tayari kwa mialiko yoyote unaweza wasilina nami kupitia namba hii

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nikiamini kuwa utaguswa na kubarikiwa zaidi kila wakati utakapokuwa unasikiliza wimbo huu, Bwana Yesu asifiwe!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Gift Mwamba kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 714 693 768 au +255 744 775 991
Facebook: Gift Mwamba
Instagram: @mwambagift
Youtube: Gift Mwamba

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top