Connect with us

Get Up Youth Over Night Kufanyika Tar 16 June Ngaramtoni Arusha.

Uncategorized

Get Up Youth Over Night Kufanyika Tar 16 June Ngaramtoni Arusha.

Mkesha mkubwa wa kusifu na kuabudu pamoja na mafundisho ya neno la Mungu uliopewa jina la Get Up Youth Over Night itafanyika katika maeneo ya chuo cha Habari Maalum Ngaramtoni mkoani Arusha.

Mkesha huo umeandaliwa na The Annointed Melodies pamoja na chuo cha habari maalum Arusha lakini utawashirikisha waimbaji na vikundi mbalimbali kutoka maeneo tofauti.

miongoni mwa waimbaji na vikundi vitakavyohudumu katika mkesha huo ni pamoja na kundi kongwe na maarufu la mziki wa injili Tanzania wanajulikana kama New Life band lakini pia watakuwepo PICASF kutoka chuo cha uhasibu Njiro Arusha, Rhema Worship Team Kutoka FPCT kimahama Arusha mjini ,machalii wa Yesu pamoja na wenyeji Annointed Melodies.

Lakini waimbaji binafsi ni pamoja na kijana anaefanya vizuri hivi sasa na nyimbo zake amenifanyia amani pamoja na wimbo kutoka Dar es salaam anaitwa Paul Clement , lakini pia mshindi wa Gospel Star search ukanda wa kaskani Kelvini Weber wengine ni Andrew Beda kutoka Dar ,Shadrack Robert kutoka Arusha, Saimon Rweikiza kutoka Arusha na wengine wengi. lakini pia kutakuwa na mafundisho ya neno la Mungu toka kwa watumishi Pastor Titus Mumo na Apostle Shemeji Melayeki na pia  commedy kutoka  the Swahili Brothers, Faithful Sizya, Jovity Benaventure, na dancers from FDG Dancers.

Watu wote wa Arusha na maeneo ya karibu mnakaribisha kushiriki katika mkesha huu ambao unatarajiwa kuwa wa tofauti sana. Kwa mawasiliano zaidi na namna ya kufika, unaweza kupiga simu namba +255 752 948 754 au +255 758 122 607.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

More in Uncategorized

To Top