Habari

Geraldine Oduor Mwimbaji kutoka Nchini Kenya Awashauri Waimbaji wa Tanzania Namna ya kutunza Talanta zao.

Geraldine Oduor ametoa ushauri wake juu ya waimbaji wa Tanzania namna ya kutunza vipaji vyao walivyopewa na Mungu na kuacha kujichanganya changanya.

Akizungumza na GospoMedia alisema kuwa Watanzania ni watu waliobarikiwa sana kiuimbaji na namna sauti zao walivyobarikiwa ni za tofauti na waimbaji wengine ambao huwa tunawasikia toka mataifa mengine.

Nawapongeza sana ila kama wakristo wenzangu mahali popote pale ulimwenguni nina washauri wasiimbe tu kisa wanatalanta na sauti nzuri ila wawe wakamilifu kwa kufuata maagizo ya Mungu wanaomuimbia  isiwe tu kwa kuimba ila kwa matendo pia wasimame na wokovu kikamilifu na ndio iwe funzo na ushuhuda kamili usio leta aibu kwa mwili wa kristo na kwa waimbaji wote wa Injili ningeshauri tufanye kazi ya Bwana tukimtegemea yeye na Mungu ndiye huinua na kushusha mtu hivyo kama umeinuliwa usije ukawadharau wenzako“Alisema

Aidha aliongeza na kusema kwamba”kwani siku yao na wao inakuja ya kuwa juu kama ulipo wewe hapo leo kwa unyenyekevu na upendo uwakubali wanaoibuka bila kutarajia malipo yoyote kwani Mungu ndiye Mpaji na kwa wale au kutafuta mpenyo mtegemee Mungu tuu ndiye wa kuinua usidanganyike kutafuta njia za mkato ili uweze kupanda kwani kisichojengwa juu ya mwamba ambaye ni Yesu kitabomolewa muda kidogo kilichojificha kitafichuliwa na Tabia njema ni muhimu kuliko Umaarufu”Alisema Geraldine Oduor.

Mwimbaji huyo ambaye mpaka sasa ana albamu tano na anatamba na wimbo wake aliomshirikisha Christina Shusho wa Tanzania uitwao Napenda.

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko na mwimbaji Geraldine Oduor wasiliana naye kupitia:

Facebook: Geraldine Hephzibah Oduor
Simu/Whatsapp: +254 795 535 753
Email: geraldineoduor@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Tazama Picha kumi za Mwimbaji Rogate Kalengo akiwa katika pozi tofauti.

Next post

Habari Picha za HILASTERION Tarehe 18-19 February. Jijini Arusha Hizi Hapa.