Habari

From Facebook: Mch.Peter MitiMingi: Wakristo Wanaongoza kwa kutokujua kufanya Tendo la Ndoa.

Katika Ukarasa wake wa facebook,Mchungaji Mitimingi ameandika,
WAKRISTO HASA WALOKOLE WANAONGOZA KWAKUTOKUJUA KUFANYA TENDO LA NDOA KWA KIWANGO NA UFASAHA.
Vijana mkipofuka macho mimi simoooo!!
Wakristo na hasa walokole ndio wanaoongoza kwa tatizo za kutojua kufanya tendo la ndoa kwa kiwango. Wakristo wengi hulichukulia tendo la ndoa kama kitu kichafu na cha kidunia na cha hovyo hovyo. Tendo la ndoa katika ndoa ni ibada kamili kwa wanandoa. Si kitendo kiovu ni kitendo kitakatifu cha Kimungu halisi kwani kinatokana na Mungu. Kinakuwa kiovu na cha dhambi kinapofanyika nje ya ndoa hapo tendo la ndoa hubadilika nakuwa uzinzi au uasherati kwa wasio na ndoa. Hapo ndipo kuna tatizo kwa walokole. Walokole ndio wanaongoza kwa kutokujua kufanya tendo la ndoa kwa ufasaha. Kwa nini hawajui ni kwa sababu hawajifunzi. Wanajifunza habari za Roho Mtakatifu, wanajifunza kunena kwa lugha na wanaishia hapo. Ukiingia kwenye ndoa hujui la kufanya. Mwanamke huji wapi utamshika mumeo ili asisimke kadhalika na mwanamume. Mlokole wa kike akiwa kiatandani na mume wake wakati wa tendo la ndoa unakuta kajilaza chali tu kama gogo anasikilizia mume wake akiangaika. Yeye ndo kwanza katulia tuli kama maji mtungini. Ukija kwenye namna ya kuaandaaani kwajili ya tendo la ndoa hapo utaona ni sifuli. Ukija kwenye mitindo hapo ni sifuri walolole wana mtindo wao mmoja tu wa KIFO CHA MENDE tu tokea mwanzo wa ndoa yao mpaka sasa wanawajukuu mwendo ni huo huo wa kifo cha mende tu, wakati ipo mitindo 112 tofauti tofauti.
KITABU HIKI CHA THAMANI YA TENDO LA NDOA KINAPATIKANA KATIKA OFISI ZA VHM MWENGE DSM.

Advertisements
Previous post

Audio Song: Moyo Wangu by Bonnie Prince Nzogere.

Next post

Bishop Nickodemus Shaboka: Comedy kanisani isivuke Mipaka.