Audio: Frida Felix Feat. Paul Clement, Allan Pyuza - Wakati - Gospo Media
Connect with us

Audio: Frida Felix Feat. Paul Clement, Allan Pyuza – Wakati

Audio

Audio: Frida Felix Feat. Paul Clement, Allan Pyuza – Wakati

Baada ya kimya cha muda mrefu toka alipoachia wimbo uitwao “Nimemchagua Yesu” kutoka kwenye albamu yake iitwayo Neno aliyoiachia mwaka 2017, mwimbaji Frida Felix kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameachia wimbo wake mzuri kabisa uitwao WAKATI akiwa amemshirikisha mwimbaji mahiri Paul Clement pamoja na Allan Pyuza. Muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza John Honore kutoka ndani ya studio za Amen Voice Records.

WAKATI ni wimbo uliobeba ujumbe wa matumaini na kuhamasisha watu waliokata tamaa, kupitia wimbo huu mwimbaji Frida anatukumbusha kuwa katika maisha yetu wanadamu ni lazima tupitie nyakati tofauti ili tuweze kuwa imara na kuwa karibu zaidi na Mungu ili tuweze kutambua majira na nyakati hasa zile ngumu ili tuweze kuzishinda haijalishi kuwa ni nyakati ngumu kwa kiasi gani tunachopaswa kutambua kuwa kila jambo lina Wakati wake, wewe ambaye kwasasa unapita katika mazingira magumu amini katika Mungu kuwa kuna wakati furaha unakuja kwa ajili yako, utapokea baraka zako kama ulivyo ahidiwa.

“Wimbo #WAKATI unahusu mtu ambaye anatagemea kupokea Baraka za Mungu, kwamba wakati ni sasa, asiangalie mazingira yanaashiria nini, watu wanasema nini, Bali azikiri Baraka alizoahidiwa na Mungu, Maana kuna nguvu katika Imani iliyondani ya mtu na ukiri” – Alisema Frida

Nina imani kuwa utapokea nguvu na baraka nyingi kila utakapokuwa unasikiliza wimbo huu, Karibu usikilize na  Bwana atakubariki kama alivyoahidi kwamaana Mungu yupo upande wako, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Frida Felix kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 093 696
Facebook: Frida Felix
Instagram: @fridafelixofficial
Youtube: FridaFelixOfficial

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top