Audio

Audio: Frank Mjuni – HEYA

Baada ya kufanya vyema kupitia nyimbo zake mbili alizoachia mwaka 2017 ikiwemo ”YAHWE”na ”AINULIWE” ambazo zilifanya vyema kupitia tovuti ya gospomedia.com na kwenye vyombo vingine vya habari pia kama vile radio na blogs, na leo kwa mara nyingine tena mwimbaji Frank Mjuni anayetokea jijini Mbeya ameachia wimbo wake mwingine mpya uitwao HEYA ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Baraka chini ya mikono ya prodyuza Isa.

HEYA ni wimbo mzuri uliobeba ujumbe wa kuwakumbusha watu wanaoingia kwenye ndoa hasa vijana ambao wameamua kuishi pamoja kama mume na mke. Maandiko yanasema Waefeso 5:31 31“Kwa sababu hiyo, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja.”

”Mungu alipokuumba hakukuacha peke yako alifanya msaidizi toka ubavuni mwako akafanyike faraja siku za huzuni yako akafanyike baraka liwe tabasamu lako, Iwe kwa mvua na jua iwe kwa tabu na njaa iwe shida na raha muwe wote pamoja.” – Frank Mjuni

Ni hakika utabarikiwa na wimbo huu ambao utaufurahia na kukugusa kwa namna ya pekee hasa kwa wewe ambaye kwasasa unaingia kwenye ndoa na wewe ambaye una matarajio ya kuingia kwenye ndoa, Mungu akawe taa ya kila kitu unachotarajia kuanzia katika uchumba wako mpaka ndoa yako, ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kuhuduma wasiliana na mwimbaji Frank Mjuni kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 757 646 037
Facebook: Frank Mjuni
Instagram: @frankmjuni
Youtube: Frank Mjuni
Twitter: @frankmjuni

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: TKLEX – Miracle In The Air

Next post

Audio: Goodluck Gozbert - Hauwezi kushindana | Lyrics