Video

Music Video | Audio: Forward Mazuruse Feat. Betty Barongo – Muneni(Uko na Mimi)

Tukiwa tumebakiza saa chache kumaliza mwaka 2017 kwa mara ya kwanza leo nimekusogezea video nzuri na wimbo wenye kubariki sana uitwao Muneni(Uko na Mimi) kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Zimbabwe akifahamika kwa jina la Forward Mazuruse akiwa amemshirikisha muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Betty Barongo, video ikiongozwa na director kutoka studio za Key Arts Films na muziki ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Crixocrix.

Uko na Mimi ni wimbo ulioimbwa katika lugha ya kizimbabwe na kiswahili ukiwa ni wimbo pekee uliobeba ujumbe wa matumaini kwako wewe mwana wa Mungu ambaye kwa namna ama nyingine upo katika hali ya kukata tamaa na kuumizwa ndani ya moyo wako kutoka na shida mbalimbali ambazo zinakusumbua lakini kupitia wimbo huu naamini utapokea faraja ya uponyaji wa roho na nafsi yako iliyosinyaa na moyo uliovunjika.

Licha ya matatizo na changamoto unazopitia sasa lakini Mungu bado anampango na wewe hajakuacha unachopaswa kufanya ni kukaa miguuni pake na hakika Yesu atafungua mlango mpya wa furaha na amani katika maisha yako. Amini Mungu yupo nasi wakati wote, hata kama kuna muda tunajiona wapweke sababu ya changamoto mbalimbali ila bado Mungu yupo nasi na anatuwazia mema, Tumalize mwaka huu huku tukiamini Mungu yupo nasi na 2018 ataendelea kua nasi katika heri na baraka zote Ameen.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na wimbo huu mzuri kutoka kwa watumishi hawa wa Mungu na hakika utabarikiwa na kuinuliwa. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu wimbo huu na mialiko ya huduma ya muimbaji Foward Mazuruse wasiliana na muimbaji Betty Barongo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 768 803 740
Facebook: Betty Barongo
Instagram: @bettybarongo
Youtube: Betty Barongo

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Video | Audio: Anicia Kinemo - Ninakuabudu

Next post

Nyimbo 100 Bora 2017