FINISHING WHAT YOU STARTED SOMO KUTOKA KWA MCHUNGAJI ELLY DAVID. - Gospo Media
Connect with us

FINISHING WHAT YOU STARTED SOMO KUTOKA KWA MCHUNGAJI ELLY DAVID.

Mafundisho

FINISHING WHAT YOU STARTED SOMO KUTOKA KWA MCHUNGAJI ELLY DAVID.

Shalom leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tumekuletea video ya somo kutoka Mchungaji Elly David kutoka Tanzania somo hili linahusu kuwapa matumaini na kuwatia moyo vijana na watu mbalimbali kumaliza mambo au vitu walivyovianza kama wewe ni kijana na umeanza kufanya kitu flani ambacho umeona kweli Mungu ndipo alipokubariki kufanya kitu hicho au jambo hilo basi ulifanye kwa juhudi na maarifa yako yote mpaka kufikia kusudi la Mungu lakini katu usiache kuendelea kufanya jambo hilo kwakuwa hapo ndipo Mafuta yako ya baraka yalipo hakika kupitia video hii yenye maneno mafupi kutoka kwa Mchungaji Elly David utaweza kubarikiwa sana na  kukusaidia kukupa mwanga wa Matumaini mapya juu ya sauti ya Mungu kwako wewe Kijana.

Elly David ni kijana na ni Mchungaji wa kimataifa, ambaye alianza kuhubiri injili katika umri mdogo sana na kadri alivyokuwa anaendelea kukua alianza huduma ya kuhubiri Injili katika mitaa mbalimbali kwa kufanya mikutano na semina na mpaka kufikia sasa ameweza kuanzisha na kuendesha vipindi vya Radio na TV sehemu mbalimbali duniani ambapo kupitia mahubiri yake Mungu amempa kibali cha kubadilisha Maisha ya watu sio tu Afrika lakini pia katika nchi nyingi duniani.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuzungumza na Mchungaji Elly David kupitia namba +255688440029, Email:keepthedream.david@gmail.com, au pia unaweza kuwasiliana naye kupitia mitandao ya kijamii Facebook: Elly David, Instagram: @ellydavid1 YouTube: Elly David

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA instagram: @gospomedia

More in Mafundisho

To Top