Habari

Fergie wa Kundi la Black Eyed Peas Aonekana Kuhudhuria Kanisani.

Fergie, mwimbaji mkuu wa bendi maarufu ya Black Eyed Peas, hivi karibuni ameonekana kuhudhuria kanisani katika wiki chache zilizopita. Kwa mujibu wa gazeti la Christian Today, Muimbaji huyo mwenye asili ya Los Angeles alionekana kuhudhuria huduma ya kanisani hapo akiwa na mumewe pamoja na mtoto wao mwenye umri wa miaka 3, anayefahamika kwa jina la Axl. Wanandoa hao walioana mwaka wa 2009, na muimbaji huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, amebarikiwa sana kuwa na mume aliyenaye.

Gazeti la Christian Today pia limekuwa likifuatilia safari ya imani ya mwimbaji huyo wakati anapambana na matumizi ya madawa ya kulevya. wakaeleza hivi:

“Fergie amegeuza maisha yake yote, kwa kuyashinda matumizi ya dawa za kulevya na kumgeukia Mungu. Katika kipindi cha televisheni kilichopita cha Oprah Winfrey, kiitwacho ‘Oprah’s Next Chapter,’ mwimbaji huyo alieleza kuwa wakati alipokuwa akiingia kanisani, alikuwa na hofu na mashaka kwamba polisi wa FBI walikuwa nyuma yake. ”

“‘Akili yangu ilinidanganya mambo mengi.  ‘Fergie alimwambia Winfrey juu ya matumizi yake ya madawa ya kulevya. ‘Nilianza kupata hofu na mashaka kweli juu matumizi yangu ya madawa ya kulevya. Kwa hiyo nilikwenda siku moja katika kanisa hili na nilifikiri kuwa polisi wa FBI na timu za SWAT zilikuwa nje ya kanisa. ”

Fergie anaamini kuwa ni Mungu ndiye aliyemkomboa kutoka kwenye mikono ya matumizi ya madawa ya kulevya. Leo, amekuwa mwanamke maarufu na aliyemstari wa mbele akiendelea na safari yake ya imani huku akazidi kupata mafanikio kupitia kazi zake.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Namba Moja ya Walter Chilambo yapokelewa vizuri

Next post

Eddah Mwampagama Mbioni Kuachia Video Yake Mpya.