Habari

Fahamu Ukuaji wa Ukristo katika nchi ya korea ya Kaskazini Licha ya Mateso makali kwa Wakristo.

Korea ya Kaskazini ni nchi namba moja inayoongoza kwa mateso mabaya zaidi kwa Wakristo, kwa mujibu wa mtandao wa Open Doors 2017 World Watch List, lakini licha ya mateso hayo yaliyokithiri kwa wakristo bado ukristo unazidi kukua, ripota mmoja alisema.

Taasisi ya Christian Post ilitoa taarifa kuwa bwana mmoja aitwaye Kim Chung-seong aliweza kutoroka kupitia upande wa kulia wa Korea Kaskazini kwa kuhofia kuuawa na wana usalama wa nchi hiyo na kwasasa anaishi nchini Korea Kusini na kushiriki katika kazi za kimisionari.

“Jambo moja ambalo utawala wa Korea Kaskazini unahofia zaidi ni kuenea kwa Injili,” alisema bwana Kim Chung-seong Ijumaa ya wiki iliyopita wakati alipohudhuria katika mkutano wa kwanza wa Dunia wa mwaka wa ulinzi wa wakristo katika mji wa Washington, DC nchini marekani.  Alisema “Kwa sababu Biblia na Injili inaongea ukweli, na mwanga huangazapo kwenye chumba chenye giza, kutakuwa na mwanga katika chumba. “

“Wapo tayari kufanya chochote kuzuia kuenea kwa Injili katika nchi ya korea ya kaskazini lakini kama unavyoweza kuona, hatuwezi kuzuia jua kwa mikono yetu.” Aliendelea.

Kim Chung-seong upande wa kushoto

Alisema kuwa Wakristo katika nchi ya Korea ya Kaskazini wanalazimika kuficha imani yao dhidi ya serikali na wakati mwingine hata familia zao wenyewe ili kuepuka mateso makali.

Uchunguzi na msako wa wakristo upo siku zote katika nchi hii ya korea kaskazini na Wakristo wanahitaji kuwa makini sana kwa kutokuangalia vile wanavyoabudu au kujihusisha na aina zingine ya shughuli za kidini.

“Kuabudu chama tawala cha raisi Kim Jong na familia yake ni lazima kisheria kwa wananchi wote, na wale ambao watashindwa kuzingatia sheria hiyo (ikiwa ni pamoja Wakristo) watakamatwa, kufungwa, kuteswa au kuuawa. Familia yoyote ya Kikristo inaenda jela na kufanyishwa kazi ngumu katika makambi ya mateso, ambapo mpaka sasa haijulikani ni idadi ya watu wangapi wanakufa kila mwaka kutokana mateso ya kupigwa na njaa.

Kim Chung-seong

Wale ambao hujaribu kukimbilia nchi ya Korea ya Kusini kupitia China hukumbana na vikwazo hatari vya kukamatwa na kuuawa au kufungwa maisha jela, na wanaobakia nyuma mara nyingi wanakuwa hawako katika hali salama, ” ripoti inasema kutoka taasisi ya Christian persecution charity Open Doors.

Lakini licha ya vikwazo vyote hivi, mpaka sasa kuna wastani ya Wakristo 300,000 katika nchi ya Korea ya Kaskazini.

 

Kwasasa taasisi ya Kim Chung-seong inajihusisha na huduma ya kutangaza ujumbe wa Injili, muziki wa Injili, na habari za ulimwengu ndani ya nchi ya korea kusini ili kufikia wananchi wake.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Ndoa: Fuata Mwongozo wa Mungu ili Uwe na Ndoa Yenye Furaha.

Next post

Download Music Audio: David Madaha Feat Suzy Madaha - Ulimwengu wa Leo