Uncategorized

FAHAMU NCHI 11 ZENYE WATU WENGI WASIOAMINI UWEPO WA MUNGU.ISRAEL IKIWEMO

Atheism ni wazo la kukataa uwepo wa Mungu/miungu. Neno Atheism limetokana na neno la kigiriki (atheos) “bila mungu”. Mtu wa kwanza kujiita “atheist” (asiyeamini uwepo wa Mungu) alikuwepo katika karne ya 18.
Kumekuwa na mabishano yaliyotoka katika falsafa kufanywa kuwa ya kijamii na kihistoria. Imezua utata wa kutoamini uwepo wa Mungu kwa vigezo kama, hakuna uthibitisho wa kuonekana, tatizo la uovu ufanywao kutokana na dini n.k.
Je ni nchi gani yenye watu wengi wasioamini uwepo wa Mungu?
Katika historia watu wasiomini uwepo wa Mungu walichukuliwa kama waabudu shetani, lakini leo hii mtu ana uamuzi wa kuchagua kuwa na dini ama kutokuwa nayo bila kuathiri mahusiano yake na watu wengine.

Kutokana na Worldwide Independent Network. 63% ulimwenguni ni watu walio na dini. Na upande mwingine kati ya 11 mpaka 13% ni wasioamini uwepo wa Mungu (atheists) na 22% hawana dini. Fahamu kuwa kuna utofauti kati ya watu wasio na dini na wasioamini uwepo wa Mungu/miungu (atheists). Wasio na dini hawahitaji kufuata sheria za dini lakini hawapingi uwepo wa Mungu, lakini atheists hawaamini uwepo wa Mungu na dini pia hawaiamini.
Husema atheism siyo dini au mpango wa kutoamini na hawana mpango wa kutaka kuwashawishi watu kutoamini kama wao.shutterstock_215094925-750x499 (1)

Hizi ndizo nchi 11 zenye watu wengi wasioamini uwepo wa Mungu (Atheism).
11. ISRAEL atheists ni 3.028.320 (36%). Wengi ni Wayahudi.
10. HONG KONG ni 3.795.272 (52%). Asilimia kubwa na Hong Kong ni wasio na dini na atheists. Hesabu ziingine zimeonyesha atheism inaweza kuwa 90%.
09. SWEDEN ni 4.515.666 (46%) ni nchi inayojulikana kwa asilimia kubwa ya wakazi hawana dini.
08. CZECH REPUBLIC ni 5.479.666 (52%) Taifa hili limegundua uchache wa watu walio na dini. Pia watu wengi hukataa kujibu kama wana dini ama hawana, huenda walio na dini wakapungua zaidi siku za usoni.
07. NETHELANDS ni 6.769.320 (40%). Mpaka kufikia karne ya 20 Ukristo ulikuwa umeenea sana. Lakini watu wengi sana wamehamia atheism (kutoamini uwepo wa Mungu) na tutegemee siku za usoni ongezeko kubwa. Ni moja ya nchi zenye watu wengi wasio amini uwepo wa Mungu.
06. UNITED KINGDOM ni 25.920.000 (40%). Asilimia kubwa ya Wanawake ni ateists. Pia wazee wengi ndiyo waamini lakini Vijana ni atheists au hawana dini.
05. Ufaransa ni 27.505.670 (41%). Watu wengi Ufaransa ni atheists na wanostiki. Katika makala nyingi Ufaransa huwa kwenye top 10 kwa wingi wa atheists na wanostiki.
04. Vietnam ni 30.837.840 (33%). Vietnam ni nchi inayojulikana kuwa ni nchi ya wasioamini uwepo wa Mungu (Atheism), imezoeleka watu wan chi kuabudu mababu zao ambayo inaitofautisha nchi hii na zingine.
03. Ujerumani ni 30.855.050 (38%). Ujerumani ya mashariki ilikuwa na watu wengi wasio na dini. Kwa sasa namba ya walio na dini inaongezeka.
02. Japan ni 58.342.720 (46%). Japan ni nchi isiyo eleweka kwakuwa mtu mmoja aweza kuwa na dini zaidi ya moja na pia hawaelewi wala kufuata sheria za dini yoyote.
01. China ni 1.029.390.000 (75%). China ndiyo nchi yenye watu wengi duniani, kwahiyo siyo ajabu kuwa na namba kubwa ya watu wasioamini uwepo wa Mungu (Atheism). Baadhi ya sehemu 90% ni wasioamini uwepo wa Mungu (Atheists). Na nchi pia ina wasioamini uwepo wa Mungu wengi (Atheists) na wachache sana wanao amini.

Imeandaliwa na Douglas Kyungay, +255719 915 008

Advertisements
Previous post

EXCLUSIVE: HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA

Next post

DOWNLOAD AUDIO SONG: BWANA TUNAOMBA-B ZABLON SENIOR