Audio: Fabian Fanuel Feat. Goodluck Gozbert - Hufananishwi - Gospo Media
Connect with us

Audio: Fabian Fanuel Feat. Goodluck Gozbert – Hufananishwi

Audio

Audio: Fabian Fanuel Feat. Goodluck Gozbert – Hufananishwi

Baada ya ukimya wa Miaka 8 Mwaka 2016 FABIAN FANUEL mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania ameamua kurekodi na kuachia singo yake mpya aliyomshirikisha mwimbaji Goodluck Gozbert kutoka Mwanza Tanzania.
Akiongea na GospoMedia, Fabian Fanuel amesema kuwa aliamua kufanya kolabo na Goodluck Gozbert akiamini kuwa wimbo huu utafanya vizuri na kwa kweli anamshukuru Mungu kwa kumpa wimbo mzuri ambao unamzungumzia Mungu mwenyewe… Fabian ameongeza kuwa kwa sasa anafanya maandalizi ya kuachia albam yake mpya inayoitwa MUNGU HAFANANISHWI hivyo anaomba watanzania wampokee na wampe sapoti ya kutosha ili afike kwenye hatma ambayo Mungu amepanga.
Fabian Fanuel ametuambia pia kuwa yeye yuko tayari kwa mialiko na kwa sasa anafanya kazi Kwa Neema Fm Radio 98.2 Mwanza na Pia ni Reporter wa Clouds Tv na Cloud Fm Mwanza. kwa lolote kuhusu yeye unaweza kuwasiliana na Fabian Fanuel kwa namba yake ya simu +255655 0284000 au +255767028400. Barikiwa sana!!

More in Audio

To Top