AudioVideo

Video | Audio: Eunice Kemunto – Moyo Safi

Kutoka nchini Kanada mpaka Tanzania kwa mara ya kwanza leo tunamtabulisha kwako mwimbaji mpya katika huduma ya muziki wa Injili Afrika anayefahamika kwa jina la Eunice Kemunto ambaye hivi karibuni ameachia video yake ya kwanza kwa mwaka 2018 iitwayo Moyo Safi, Video hii imeongozwa na director Einxer kutoka studio za Maxum Vision.

“Mathayo 5:8 Heri wenye moyo safi, maana watamwona Mungu

Moyo Safi ni wimbo wa Ibada(Maombi), Nikimuomba Bwana anitengeneze ili niwe na Moyo safi, Ni wimbo unaonikumbusha mimi pamoja na wote watakaosikiliza wimbo huu kwamba ikiwa tunatafuta kwanza ufalme wa Mungu, Basi tuwe na hakika kwamba vitu vyote vingine tutazidishiwa, Kama neno la Mungu lisemavyo kutoka katika kitabu cha Mathayo 6:33 Bali, shughulikeni kwanza juu ya ufalme wa Mungu na matakwa yake, na hayo yote mtapewa kwa ziada.” – alisema mwimbaji Eunice

Ni imani yetu kuwa utabarikiwa na kuinuliwa kila utakapokuwa unatazama video hii njema na wimbo huu ukawe sehemu ya kukumbusha na kukutengeneza Moyo wako uwe safi na wenye kunyenyekea mbele za Bwana, Ameen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Eunice Kemunto kupitia:
Simu/WhatsApp: +1 7809 010 912
Facebook: Eunice Kemunto
Instagram: @kemunto_eunice
Email: eunicemarube@gmail.com
Youtube: Eunice Kemunto

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Liza J-Umenifurahisha

Next post

Ritha Komba Aachia Rasmi Albamu ya Ni Rafiki