Video | Audio: Eunice Kemunto - Mambo ya Ajabu - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Eunice Kemunto – Mambo ya Ajabu

Audio

Video | Audio: Eunice Kemunto – Mambo ya Ajabu

Baada ya kuachia video ya wimbo wa Ibada uitwao Moyo Safi mwezi Agosti na kuendelea kufanya vizuri, Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kanada Eunice Kemunto amerudi tena kwa kuachia video yake ya pili iitwayo Mambo ya Ajabu.

Video hii imeongozwa na director X-Antonio, Muziki ukiwa umetayarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Teddy B kutoka nchini Kenya.

“Wimbo huu umeandikwa kutoka kwenye kiini cha sifa, Ninamsifu Bwana kwa miujiza ambayo amefanya katika maisha yangu, Kila siku ninayoishi ninaendelea kuona miujiza, Hata vile tuamkapo kila asubuhi hakika huo ni muujiza, Kupitia wimbo huu ninamhimiza kila mmoja kuja pamoja na kumsifu Bwana kwa miujiza yote, ishara na maajabu ambayo anafanya.

Kama vile Paulo na Sila ambao waliomba na kusifu usiku kucha ndipo Mungu alifurahi na kuvunja milango ya gereza na kuwaachilia. Hivyo wewe kaka na dada yangu mpendwa naomba upokee wimbo huu, Ni maombi yangu kwamba kupitia wimbo huu sisi sote tutapata sababu ya kumsifu Mungu kila siku, Kwa maana sifa zinapokwenda kwa Mungu ndivyo miujiza ya baraka hushuka na kutokea, Ubarikiwe!” – alisema Eunice Kemunto.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema ambayo ni hakika itakubariki na kukupa jambo jipya ndani yako, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Eunice Kemunto kupitia:
Simu/WhatsApp: +1 7809 010 912
Facebook: Eunice Kemunto
Instagram: @kemunto_eunice
Youtube: Eunice Kemunto

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top