Audio

Audio: Erick Lenjima Feat. Cecilia & Exavery – Unconditional Love

Baada ya kufanya vizuri mwaka 2017 kupitia nyimbo zake mbili alizoachia ikiwemo “Usinipite” na “Impossible”, Kutoka mjini Moshi, leo kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 nakukaribisha kusikiliza wimbo mpya uitwao “Unconditional Love” kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa Hip-Hop anayefahamika kwa jina la Erick Lenjima akiwa amemshirikisha mwanadada Cecilia Mdota na Exavery Geofrey. Wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Range93 na W&M Production chini ya mikono ya prodyuza Capacity.

“Unconditional Love ni wimbo uliobeba ujumbe juu ya upendo mkuu wa Mungu kwetu sisi wanadamu bila kujali tofauti zetu hali zetu na mabaya au maovu tunayoyatenda . Unconditional Love ni wimbo unaoelezea hali mbalimbali ambazo mwanadamu anapitia na kumsahau Mungu lakini bado Mungu anatupenda na yupo tayari kutupokea muda wowote . Upendo wa Agape wa Mungu usio na kipimo #Unconditional Love” – Lenjima

Rapa Lenjima kwasasa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha ushirika Moshi MoCu ambaye mbali na kuimba lakini pia ni mtunzi na mwandishi mzuri wa nyimbo za Injili.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri wenye ujumbe unaoweza kubadilisha maisha yako siku ya leo. Barikiwa!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na Lenjima kupitia:
Simu: +255 679 381 299
Facebook: Erick Lenjima
Instagram: @erick_lenjima

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Isioma - This is me

Next post

Audio: Peter Mdoe - Asante