Video: Erick Kisindja Feat. Natasha Lisimo - Ayubu - Gospo Media
Connect with us

Video: Erick Kisindja Feat. Natasha Lisimo – Ayubu

Video

Video: Erick Kisindja Feat. Natasha Lisimo – Ayubu

Kutoka jijini Nairobi Kenya kwa mara ya kwanza leo tumekusogezea video nzuri na iliyobeba ujumbe wa pekee inayokwenda kwa jina la Ayubu kutoka kwa mwimbaji na mhubiri anayefahamika kwa jina la Erick Kisindja mwenye asili ya nchini Kongo hapa akiwa amemshirikika mwanadada mwenye sauti ya pekee kutoka nchini Tanzania maarufu kama Natasha Lisimo.

Video hii imeongozwa na Rehoboth pictures, Muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa chini ya mikono ya prodyuza Mujwahuki.

“Pamoja na kupitia mapito mengi katika maisha yake Ayubu, aliweza kuvumilia na kuzidi kumwamini Mungu mpaka dakika ya mwisho na hata kurudishiwa zaidi mali zilizoharibiwa.

Hakika Ayubu alikuwa Mtumishi wa Mungu mwanifu sana.. katika video hii kuna igizo la mfano wa mke wa Ayubu ambaye imani yake iliyumba sana kutokana na majaribu waliyopitia na kumwambia Ayubu mkufuru Mungu na ufe, lakini Ayubu hakuyumba aliendelea kumwamini Mungu.. Hakika tunajifunza kitu hapa, tusikate tamaa sababu ya majaribu tuzidi kumwamini Mungu siku zote maana majaribu ni mtaji wa kukuza imani,  MUNGU AKUBARIKI SANA.” – Erick alisema

Mwimbaji Erick amefanikiwa kuachia album ya kwanza inayokwenda kwa jina la Ninaye Yesu na sasa anatarajia kuachia album ya pili inayokwenda kwa jina la Mchungaji Mwema.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii iliyobeba ujumbe mzito na hakika utajifunza na kuweka jambo jipya ndani yako, Amen.

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mtumishi wa Mungu Erick Kisindja kupitia:
Simu/WhatsApp: +254 706 234117
Facebook: ERICK Kisindja | Natasha Lisimo
Instagram: @henriquesdasilva | @natashalisimo

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top