Video

Video | Audio: Entujael Msangi – Upendo wa Kweli

Kutoka kwenye albamu yake mpya inayobebwa na jina la Sababu ya Kumwabudu iliyo katika mfumo wa DVD muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania leo anakukaribisha kutazama moja ya video inayopatikana kwenye albamu hiyo ambayo kwasasa ipo sokoni. Video hii inaitwa Upendo wa Kweli ikiwa imeongozwa na director Joe.

Wimbo huu unaelezea, kukumbusha na kuhimiza juu suala la Upendo wa kweli baina ya wanadamu na Mungu ambaye kwa hakika ukitazama matendo yake unagundua kuwa upendo wake ni wa kiwango cha chuu sana hivyo kupitia wimbo huu mtumishi wa Mungu Entujael anatukumbusha kuwa upendo wa kwanza unapatikana kutoka kwa Mungu kwenda kwa wanadamu na upendo wa pili ni ule unaopatikana baina ya binadamu wenyewe lakini upendo wa kweli unapatikana kwa Mungu peke yake kwakuwa upendo wa binadamu una kikomo chake. Baba, Mama, Mke, Mume anaweza kukupenda kweli lakini inapotokea yeyote kati ya hao amekutoka duniani hakuna atakayeweza kusimama katika upendo wa kweli zaidi ya Yesu peke yake, Hivyo ni vyema kila mwenye pumzi akafahamu namna ambavyo anaweza kuwa karibu na Mungu na kumpenda Yesu kwa maana yeye ndiye kimbilio pekee kwa matatizo na shida zetu, upendo wake hauchunguziki.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina hakika utakubariki sana, Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Entujael Msangi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 756 557 731
Facebook: Entujael Msangi
Instagram: @entujaelmsangi
YouTube: Entujael Msangi
Twitter: @entujaelmsangi

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio: Elvis Kiwanga - Showers of Blessings

Next post

Audio: The Rythm Tz - Yesu Unipendaye