Music

Music Audio: Entujael Msangi – Mwaka Huu

Heri ya mwaka mpya mwana wa Mungu! leo kwa mara ya kwanza nimekuletea wimbo wa baraka uitwao Mwaka Huu kutoka kwa mtumishi wa Mungu Entujael Msangi muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Lucky records.

Mwaka Huu ni wimbo wa shukrani unaotukumbusha kumshukuru Mungu kwa kutuvusha mwaka 2018 salama kwa maaa kuna wengi ambao walitamani kufika leo lakini hawakuweza kuifikia hivyo ni neema ya Mungu iliyotuwezesha mimi na wewe kuendelea kuwa na pumzi leo inayotufanya kusherehekea mwaka mpya 2018.

Hata hivyo kupitia wimbo huu muimbaji Entujael Msangi anasisitiza na kutamka baraka katika mwaka huu ambao anaamini utakuwa ni mwaka wa mafanikio na baraka na hata wewe ambaye unahisi bado kuna mambo ambayo umeshindwa kukamilisha mwaka uliopita basi leo una nafasi pekee ya kumshukuru Mungu na kutamka baraka katika maisha yako yale yote abayo ulishindwa kuyafanikisha mwaka uliopita basi muombe Yesu akutie nguvu ya kuweza kuyakamilisha na kusonga mbele.

”Natanguliza shukurani maana bado mpaka leo hii napumua naamini wapo watu wengi walipanga mipango yao mwaka uliopita lakini haikutimia ila ni jambo la kumshukuru Mungu ikiwa mimi na wewe bado tupo hai na hii ni kwa Neema yake Mungu Baba, Heri ya mwaka mpya.”  –  Alisema Entujael Msangi

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kwa mara ya kwanza kusikiliza na kupakua wimbo huu kwa mwaka 2018 na nina hakika utabarikiwa sana na mwaka Mwaka huu uwe wa baraka kwako, Ameen!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Entujael Msangi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 756 557 731
Facebook: Entujael Msangi
Instagram: @entujaelmsangi
YouTube: Entujael Msangi
Twitter: @entujaelmsangi

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Video 100 Bora za Muziki wa Injili Zilizofanya Vizuri 2017 Afrika Mashariki

Next post

Music Video | Audio: Eliakim James Feat. Peace Simon - Zaidi Ya Yote