Connect with us

Music Audio: Enea Mahenge – Sikati Tamaa

Muziki

Music Audio: Enea Mahenge – Sikati Tamaa

Kutoka jijini Dar es salaam kwa mara nyingine tena leo nimekusogezea wimbo mpya uitwao Sikati Tamaa kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Enea Mahenge, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Masai Records chini ya mikono ya prodyuza George Emil na Yz Manamba.

”Katika nyakati tofauti utasikia mtu anakwambia usilie nyamaza bila kujua kwamba kuna nyakati zingine  tunazipitia zinatutoa machozi, na huwa ni vigumu sana kuzuia machozi au uchungu moyoni. Katika wimbo huu namkumbusha mwana wa Mungu ambaye atapata nafasi ya kusikia wimbo huu kwamba siku zote za maisha yake hapaswi kukata tamaa, Hata kama ana machozi yatiririkayo kama mto aendelee nayo tu kwakuwa Mungu anafahamu hitaji la moyo wake na hakika siku moja atamfuta machozi yake na furaha yake itarudi ikiwa imebeba ushuda mkubwa wenye kurudisha sifa na utukufu kwa Mungu. Usikate tamaa wakati ungali hai, hiki ndicho ninachotamani asikie mpendwa aliyekata tamaa, anayelia, aliyeumizwa na kuteswa. AMINA” – Enea Mahenge

Kupitia wimbo huu naamini utabarikiwa na kuinuliwa na kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu hapa. Karibu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Enea Mahenge kupitia:
WhatsApp: +255 759 554 943
Facebook: Enea Mahenge
Instagram: @eneamahenge
Youtube: Enea Mahenge

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top