Habari

Emmauel Mbasha na Mwandishi Mbezi Watunishiana Misuli

Muimbaji wa muziki wa injili nchini Tanzania  kwa miondoko ya kufoka foka Ema Mbasha amejikuta akipishana kauli na Mwandishi wa Habari Sir Mbezi kwa madai kuwa mwandishi huyo amekuwa akimfanyia mahojiano ya umbea umbea jambo ambalo yeye hafurahishwi nalo na linamkera sana na kumshangaa mwandishi huyo kulikoni kila wakikutana lazima amhoji kuhusiana na mambo yaliyopita kwani hana habari zingine zaidi ya Umbea? alihoji Emmanuel Mbasha.

Akizungumza  kwa njia ya Simu  na Gospo Media Ema Mbasha alisema kuwa”Hana adabu, mchokonozi sana huyu mwandishi asirudie tena, nitaenda kimwili akirudia maana kila mahali nikikutana naye ana nidaka iwe kwenye Matamasha, Uzinduzi, Red Carpet yaani jamaa mchokozi sana aisee’ maswali yake ni yale yale yaani ni uchokonozi tuu mpaka nachoka asirudie tena ”Alisema na kusisitiza Emmanuel Mbasha.

Kwa upande wake Mwandishi Sir Mbezi alifafanua Mahojiano ambayo amewahi kufanya na Ema Mbasha

Mimi kiukweli sijawahi fanya mahojiano na Mbasha halafu nikafanya kama anavyonilaumu ninachokumbuka kwenye kumbukummbu zangu nikiwa na ushahidi tosha Mbasha nimemfanyia mahojiano yasiyozidi matatu kwakweli, moja na la kwanza ni kwenye uzinduzi wa Messi Chengula pale Mito ya Baraka, Fainali za Gss pale Sinza na kwenye uzinduzi wa Christina Shusho Tabata na ushahidi upo kwenye Blogs watu waingie na watazame kama kuna swali la Umbea ama uchochezi ambalo nimemhoji Mbasha na kama lipo basi mtu na acomment kwenye mahojiano hayo na kuniandikia kuwa swali fulani ni la umbea au uchokonozi, Pia nikiwa kama Mwandishi wa Gospo Media sijawahi kupost Habari za Mbasha na aliyewahi kuwa mkewe Flora ambaye kwasasa ni Madam Flora yaani sijawahi na sinaga hizo kwakweli ”Alisema Sir bezi.

Aidha aliongeza na kusema kuwa”Siku feel poa mbele za watu kuniambia maneno kama yale kwakweli, pia mimi ni mwandishi wa habari haijanipa shida saana ni sehemu ya kazi yangu so nachukulia poa hakuna mbaya Mbasha ni kaka yangu na itabaki hivyo”Alisema Mbezi

Kupishana kwa Mbasha na Mbezi kwa kauli ilitokea siku ya uzinduzi wa Mwimbaji Christina Shusho kwenye Albamu yake ya Akutende Nini? ambapo Mbezi alimwita Mbasha nje baada ya kumaliza kuimba kama ilivyo kawaida ya waandishi kwaajili ya mahojiano ndipo Mbasha alipomtolea maneno mwandishi huyo mbele ya kadamnasi kwa kumwambia aache maswali ya umbea umbea na ahoji vitu vizuri na baada ya hapo mahojiano yaliendelea bila tatizo lolote na mahojiano hayo yalirushwa moja kwa moja kupitia gospo tv.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Moses Simkoko, Sifaeli Mwabuka Wapishana Kauli Juu ya Kusheherekea Siku ya Kuzaliwa.

Next post

Muimbaji Beatrice Kitauli Ageukia Tasnia ya Comedian