Music Video | Audio: Emmanuel Mgogo - Umekusudiwa na Mungu - Gospo Media
Connect with us

Music Video | Audio: Emmanuel Mgogo – Umekusudiwa na Mungu

Video

Music Video | Audio: Emmanuel Mgogo – Umekusudiwa na Mungu

Kutoka jijini Dar es salaam, kwa mara ya kwanza leo nakukaribisha kutazama video yenye ujumbe wa kipekee kwa ajili yako mwana Mungu, video hii inaitwa ”Umekusudiwa na Mungu” kutoka kwa mtumishi wa Mungu ambaye pia ni mwimbaji mahiri na mkongwe katika kiwanda cha Muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Emmanuel Mgogo, video hii imeongozwa na studio za Touching Voice na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za JB Production chini ya mikono ya prodyuza mahiri anayefahamika kwa jina la Baraka (Smartbilionea).

”Umekusudiwa na Mungu” ni wimbo unaobeba jina la albamu yake ya tatu ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo sita katika mfumo wa DVD ambayo kwasasa inapatikana sokoni ikisambazwa na kampuni yake inayofahamika kwa jina la Mgogo Gospel Entertainment.

Moja ya kitu ambacho utajifunza kupitia video hii na wimbo huu ni uhalisia wa video yenyewe na kile ambacho mtumishi huyu anazungumzia na hiki ndicho kitu pekee kitakachokufanya usikilize na kutazama video hii mara kwa mara.

”Umekusudiwa na Mungu” ni wimbo uliobeba ujumbe wa matumaini na kuhamisha watu kuwa na imani zilizo Imara kwa Mungu ili wapate kusimama na kujitetea katika yale ambayo yanawafanya warudi nyuma na kukata tamaa kutokana na hali zao duni kiuchumi, elimu au hata nguvu zao za kiroho lakini leo mtumishi huyu wa Mungu Emmanuel Mgogo anatukumbusha na kutusisitiza kuwa Mungu ameweka kusudi kwa kila kiumbe chake hapa duniani hivyo basi kwa wewe mwana wa Mungu ambaye hujatambua basi kupitia wimbo huu utapokea mguso wa kipekee wa nguvu ya kutiwa Moyo na kuongeza ya Imani yako kwa Mungu kupitia jina la Yesu Kristo.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakuinua na kukufanya uwe kiumbe kipya chenye imani thabiti kwa Mungu kwa maana Mungu Baba ana haja na wewe, ana kusudi na wewe, jiamini.. Karibu ufurahie na ubarikiwe!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Emmanuel Mgogo kupitia
Simu/WhatsApp: +255 769 505 537
Facebook: Emmanuel Mgogo
Instagram: @emmanuelmgogo
YouTube: Emmanuel Mgogo
Email: emanuelmgogo150@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Video

To Top