Connect with us

Music Video | Music Audio: Emily Nakhungu – Umetenda

Muziki

Music Video | Music Audio: Emily Nakhungu – Umetenda

Kutoka nchini kenya, leo nimekusogezea kwako video mpya inayoitwa Umetenda kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili mwenye sauti ya pekee anayefahamika kwa jina la Emily Nakhungu.

Video hii imeongozwa na director Solomon K kutoka studio za Solomon K Image na audio ikiwa imetayaarishwa ndani ya studio za BornBlack Records.

Umetenda ni wimbo wa shukrani kutoka kwenye albamu yake mpya iitwayo Shwari na kupitia wimbo huu mtumishi wa Mungu Emily anatukumbusha kwamba kila hatua na nafasi tunazozipata leo ni kwasababu ya nguvu ya Bwana wetu Yesu Kristo hivyo sisi tukiwa kama wana wa Mungu yatupasa kumwimbia sifa na kumtukuza yeye siku zote kwa maana yeye pekee ndiye ametenda haya kwa upekee katika maisha yetu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nzuri na ni hakika itakwenda kukubariki na kukufunza jambo siku ya leo. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Emily Nakhungu kupitia
Simu/WhatsApp: +254 731 385 554
Facebook: Emily Nakhungu
Instagram: @emilynakhungu

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

To Top