Connect with us

Audio: Elvis Kiwanga – Uhimidiwe

Muziki

Audio: Elvis Kiwanga – Uhimidiwe

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Elvis Kiwanga kwa mara nyingine tena ameachia wimbo wake wa tatu kwa mwaka 2018 hii ikiwa ni baada ya kuachia nyimbo zake mbili ikiwemo “Showers of Blessings”, “Kweli” na sasa ameachia wimbo wa kuabudu uitwao “Uhimidiwe”, Muziki huu umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Dyno na kurekodiwa ndani ya studio za Dyno Records.

Uhimidiwe ni wimbo mzuri wa kuabudu uliojaa maneno ya sifa na utukufu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, Ni wimbo uliobeba maombi ya kujishusha na kuomba Rehema na Neema kwa Mungu, “Jina lako ni kuu kupita majina yote, Wewe ni Mungu mkuu na hakuna zaidi yako, wewe ni Mungu mwenye uweza Uhimidiwe.”

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu nikiamini kuwa utakwenda kuweka neno la Mungu ndani yako na kubadilisha maisha yako kuanzia sasa, Barikiwa.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Elvis Kiwanga kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 682 886 826
Facebook: Elvis Kiwanga
Instagram: @eagleredemption(Elvis Kiwanga)
YouTube: Elvis Kiwanga

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

To Top