Audio: Elvis Kiwanga - Kweli - Gospo Media
Connect with us

Audio: Elvis Kiwanga – Kweli

Audio

Audio: Elvis Kiwanga – Kweli

Baada ya kuachia wimbo wake uitwao Showers of Blessings mwezi Januari, kwa mara nyingine tena mwimbaji Elvis Kiwanga ameachia wimbo wake mpya uitwao KWELI, ikiwa ni kazi yake ya pili kuachia kwa mwaka 2018, Muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Dyno kutoka ndani ya studio za Dyno Records.

Kweli ni wimbo unaozungumzia hali ya kushuka kwa imani miongoni mwa watu wengi katika dunia ya leo, watu wengi tumekuwa hatutaki neno lenye Kweli ya Mungu na badala yake tumekuwa tunapenda kuhubiriwa na kutabiriwa mambo ambayo mara nyingi yanakuwa nje ya msingi wa Biblia kitu ambacho kinatusababisha kumkosea Mungu mara kwa mara na kutuweka mbali na uso wake, kupitia wimbo huu mwimbaji Elvis amejaribu kuzungumzia na kuwahabarisha watu kuwa dunia ya sasa imebadilika hasa katika suala la kumuamini Mungu na kutusisitiza kwamba yatupasa kumshirikisha zaidi Yesu Kristo katika roho na kweli ili aweze kutufunulia juu ya mafundisho ya kweli na uongo ili tuweze kuiepuka mitego ya shetani.

Wimbo huu umekuja kutokana na kile ambacho kipo katika ulimwengu wa kikristo kuzungukwa na watumishi wa uongo ambao wamekuwa wanaibuka kila leo na kuwapotosha waumini, yatupasa sasa tuwe makini kila mmoja awe macho katika kuongea na Mungu ili atupatie macho ya kuona, vile visivyofaa katika imani yetu.

Nina hakika kuwa kuna jambo utajifunza kupitia wimbo huu mzuri ambao utakufanya upende kuusikiliza mara kwa mara, Barikiwa mwana wa Mungu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Elvis Kiwanga kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 682 886 826
Facebook: Elvis Kiwanga
Instagram: eagleredemption(Elvis Kiwanga)
YouTube: Elvis Kiwanga

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

To Top