Videos

Music Video | Audio: Elvis Kiwanga – I Believe

Kwa mara nyingine tena katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania leo nimekuwekea video iitwayo I Believe kutoka kwa mwana wa Mungu anayefanya muziki wa Injili kwa mtindo wa kisasa(Contemporary Gospel) anayefahamika kwa jina la Elvis Kiwanga, video ya wimbo huu imeongozwa na director Jackson Joachim kutoka studio za Blessing na wimbo ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Edward kutoka studio za E Records. 

Elvis Kiwanga ni moja kati ya waaimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania walioanza kufanya vizuri mwaka 2016 kupitia nyimbo zake alizowahi kuachia ikiwemo Hakuna Mungu kama wewe, Hold onto You, Usikate Tamaa na Vumilia na mwaka huu akiwa tayari ameshaachia video yake ya kwanza iitwayo The Word(Neno) na hii ikiwa ni video yake ya pili katika mfululizo wa kazi zake anazoendelea kuachia, japo hajaweka rasmi mpango wake wa kuachia albamu yake ya kwanza aliyowaahidi mashabiki zake.

Naamini utafurahia na kubarikiwa kupitia video hii na utakapopakua wimbo huu. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Elvis Kiwanga kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 652 037 575
Facebook: Elvis Kiwanga
Instagram: eagleredemption(Elvis Kiwanga)
YouTube: Elvis Kiwanga
Email: kiwanga@outlook.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio Music: Becky Larry Izamoje – In Awe of You

Next post

Audio Music: Eliud Martine Feat Rose Francis - Tulia Kwa Yesu