Connect with us

Elly Joh: Tarehe 8 Oct 2017 ndio siku pekee Nitakayoachia pumzi yangu rasmi

Matukio

Elly Joh: Tarehe 8 Oct 2017 ndio siku pekee Nitakayoachia pumzi yangu rasmi

Dar es salaam,

Rapa mahiri wa nyimbo za Injili kutoka kundi la Borne Kingz akifahamika kwa jina la Elly Joh siku ya tarehe 8.10.2017 anatarajia kuachia albamu yake mpya inayobebwa na jina la ”PUMZI” ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo ambazo zitakwenda kugusa nafsi za watu na kuwabariki wengi.

Akiongea na gospomedia.com rapa Elly Joh amesema kuwa uzinduzi wa albamu hiyo ya “PUMZI” itafanyika katika kanisa la Wordalive Centre, Kimara baruti (Kanisa Jipya) Kuanzia saa tisa mchana na kuendelea hivyo amewasihi wadau na mashabiki wote wa muziki wake kutoka pande zote za jiji la Dar na mikoa ya jirani kuja kumpa sapoti na kumtia moyo katika kutangaza ufalme wa Mungu na kushusha Baraka kutoka kwa Mungu Baba kupitia Jina la Yesu Kristo.

Rappa Elly Joh kwasasa ameachia video yake mpya iitwayo ”Misri” ikiwa inaendelea kufanya vyema sana kupitia mtandao wa gospomedia na vyombo vingine vya habari nchini ukiwa ni wimbo wa pekee unaozungumzia ukiri wa mwana wa Mungu(Kijana) ambaye ameamua kuachana na vitendo vya dhambi na kuamua kumkabidhi Yesu Maisha yake. Kama bado hujawahi kutazama video hii, leo nakukaribisha kuitazama na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Usikose kufika siku ya uzinduzi huu na hakika utabarikiwa.

Download Audio

Simu/Whatsapp: +255 684 334 036 au 0717 057 457
Facebook: Elly Joh
Instagram: @ellyjoh
Youtube: EllyJoh

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

More in Matukio

To Top