Video | Audio: Eliud Martine - Umenikamata - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Eliud Martine – Umenikamata

Audio

Video | Audio: Eliud Martine – Umenikamata

Baada ya wiki chache zilizopita kuachia wimbo unaoendelea kufanya vizuri uitwao Siangalii Nyuma akiwa amemshirikisha mwimbaji Jesca Gazuko, Kwa mara nyingine tena mwimbaji Eliud Martine kutoka jijini Mbeya ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Umenikamata”.

Video hii imeongozwa na director Debro kutoka studio za Eagle View na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za GCM chini ya mikono ya prodyuza G Love.

“Pendo lako mkono wako wa ajabu umenifanya mimi nisiache kuja kwako Yesu ndio maana naimba wimbo wako pale nilipogundua thamini yako, Nilijikaza moyo wangu kuja kwako Yesu ili nione wema wako Yesu, Yesu ameniweka juu sana, amebadili historia yangu ya nyuma niliyotenda alinisamehe #UMENIKAMATA” – alisema Eliud

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika itakugusa na kukubariki kwa viwango vingine, Amen.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Eliud Martine kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 759 975 471
Facebook: Eliud Martine
Instagram: @eliud_martine
Youtube: Eliud Martine

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top