Connect with us

Audio Music: Eliud Martine Feat Rose Francis – Tulia Kwa Yesu

Muziki

Audio Music: Eliud Martine Feat Rose Francis – Tulia Kwa Yesu

Kutoka jijini mbeya leo kwa mara ya kwanza nimekuwekea wimbo mzuri uliobeba ujumbe wa matumaini uitwao Tulia Kwa Yesu kutoka kwa mwimbaji mpya katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Eliud Martine akiwa amemshirikisha mwimbaji Rose Francis. wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za GCM chini ya mikono ya prodyuza G Love.

Akizungumza na gospomedia.com mwimbaji Eliud Martine amesema: ”Kuna wakati moyo huumizwa na kufikia hatua ya kukata tamaa pasipo kujua kuwa Mungu yupo ambaye anaweza kubadili kila hali tunayopitia… leo kupitia wimbo huu naomba nikutie moyo kwa hali yeyote unayopitia yakupasa uuambie moyo wako utulie kwa bwana Yesu Kristo, hata kama kuna vikwazo vingi, majaribu mengi yaumizayo moyo…usitetereke na utulie kwa Yesu..maana yeye ndo tumaini la mambo yote kwetu.” – Alisema Eliud Martine

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri uliobeba ujumbe wa matumaini kwa ajili yako wewe mwana wa Mungu na nina amini utabarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na mwimbaji Eliud Martine kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 759 975 471
Facebook: Eliud Martine
Instagram: @eliud_martine
Youtube: Eliud Martine
Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top