AudioVideo

Video | Audio: Eliud Martine – Mungu Mkuu

Baada ya mwezi septemba kuachia video ya wimbo  uitwao Umenikamata, Kwa mara nyingine tena mwimbaji Eliud Martine kutoka jijini Mbeya ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mungu Mkuu”.

Video hii imeongozwa na director Debro kutoka studio za Eagle View na muziki ukiwa umetayaarishwa na kurekodiwa ndani ya studio za GCM chini ya mikono ya prodyuza G Love.

“MUNGU MKUU ni wimbo ambao unaelezea uweza, mamlaka na Ukuu ambao Yesu Kristo huutenda katika maisha yetu ya kila siku pindi tunapo pitia magumu yeye hunyoosha mkono wake wenye nguvu kutushindia kila pito, manyanyaso, masimango na vitisho vyote. Nakukaribisha mpendwa kuitazamaza video hii na kusikiliza ujumbe huu ili uweze kukuhubiria ndani ya moyo wako na maisha yako kwa ujumla.” – alisema Eliud

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii njema na hakika itakugusa na kukubariki katika viwango vingine, Amen.

Kwa watumiaji wa tovuti bonyeza hapa chini:

Download Audio

Kwa watumiaji wa App bonyeza hapa chini:
Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Eliud Martine kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 759 975 471
Facebook: Eliud Martine
Instagram: @eliud_martine
Youtube: Eliud Martine

Advertisements
Previous post

Video | Audio: Janet Otieno - Tulia

Next post

Video | Audio: Paul Clement - Mwaminifu