Video | Audio: Elandre - Mwamba - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Elandre – Mwamba

Audio

Video | Audio: Elandre – Mwamba

Baada ya kimya cha muda wa takribani mwaka mmoja toka ameachia wimbo wake uitwao Hope Alive, rapa mahiri kutoka katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania maarufu kwa jina la Elandre kwa mara ya kwanza katika mwaka 2018 ameshusha jiwe lake jipya la video ya wimbo wake uitwao MWAMBA, Video hii ikiwa imeongozwa na director anayefahamika kwa jina la Luiarts na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Kingsley(King C Music) na kurekodiwa ndani ya studio za Eternal Entertainment chini ya mikono ya prodyuza Isaac McDonald.

“Ubeti wa kwanza unaelezea ukuu wake Mungu #Mwamba ulioimara, tegemezi letu, na kimbilio letu. Na pia niligusia kwamba watu wasioamini wanavopoteza muda huko duniani au ni kwamba walioamini ndo wanawafanya waingie mitini(yani matendo yetu yanawafanya wasije kwa Yesu?) So ni angalizo tu kuwa tusimame katika nafasi zetu.

Ubeti wa pili naelezea vile najivunia kuwa ndani ya hii familia kubwa ya Ufalme wa Mungu na kuwa huu ni wakati wa kuishi maisha ya Upendo wa Mungu Baba na ku-influence hii culture(tamaduni) yetu na huo Upendo wa ki-Mungu.” – Elandre alisema

“That’s pretty much it. Otherwise hii ni aina ya miondoko ya (trap music) yani hip hop ya kizazi kipya. Wengi wanaweza wasiuelewe kwasabu hii, ila kizazi hiki naamini kinaelewa.

Video hii imefanywa na director anaitwa [Louis Shoo] @luiarts, nyimbo imetayaarishwa na @ic_tz [Isaac McDonald] wa @eternalenttz [Eternal Entertainment] na beat imetengenezwa na mdogo wake Kingsley [@kidswahili]. Kasauti katamu kwenye chorus kameimbwa na miss Neema Balige (@ms_doreen_balige). Mungu ambariki kila mmoja atakayesikiliza na kutazama video ya wimbo huu, nawashakuru sana, This is Elandre (@iamelandre). ” –  Aliongeza Elandre

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao nina imani kuwa utaifurahia na kukubariki.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na rapa Elandre kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 789 011 154 au +255 718 141 994
Facebook: iamelandre
Instagram: iamelandre
Youtube: Elandre
SoundCloud: iamelandre
E-mail: elandre819@gmail.com

Like us on facebook >> Gospo Media Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Audio

To Top