Music

Music Audio: Edwin Mrope – Unapata

Shalom mwana wa Mungu! leo kwa mara nyingine tena nimekuletea wimbo uitwao Unapata kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefanya vizuri katika kuwasilisha ujumbe wa Injili kwa mtindo wa muziki wa Singeli huyu si mwingine bali ni Edwin Mrope kutoka jijini Dar es salaam. Wimbo huu umetayaarishwa na prodyuza Flashbeatz.

Unapata ni wimbo unaohimiza watu kumtafakari Mungu kwa upya na kukana nafsi zao ili wamkubali Yesu atawale maisha yao maana vyote wanavyohangaikia duniani kwa Yesu watavipata tena katika hali ya hali ya furaha na amani itakayodumu kwako milele. ……ukitaka amani, upendo, furaha uzima kwa Yesu…. unapata..!

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utapokea habari njema na hakika utampokea Yesu Kristo ili aweze kufanya mabadiliko katika maisha yako. Karibu!!

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma  wasiliana na mwimbaji Edwin Mrope kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 246 084
Facebook: Edwin Mrope
Instagram: @edwinmrope

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Audio Music: EAGT Buzuruga - Tufurahi

Next post

Music Audio: Trusly Feat Karen - Stay With Me