Habari

Eddah Mwampagama Mbioni Kuachia Video Yake Mpya.

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka jijini mbeya Edda Mwampagama anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya ujulikanao kama Ni salama.

Akiongea na gospomedia muimbaji Edda Mwampagama amesema kuwa video hiyo itaachiwa rasmi jumapili ya tarehe 16.07.2017, video ikiwa imeongozwa na Director Einxer na wimbo ukiwa umetengenezwa ndani ya studio ya Mefo Records chini ya mikono ya producer Kingson kutoka jijini Mbeya.

Ameongeza kuwa video hiyo itakuwa ni ya kipekee sana na anaamini watu wengi watabarikiwa sana sio tu kwa video hiyo bali pia kwa ujumbe ulio katika wimbo huo, Hivyo amewaomba wadau na mashabiki wote wa muziki wa Injili wakae tayari kuipokea video hiyo iliyotayarishwa kwa kiwango cha hali ya juu.

kupitia gospo tv tumekuwekea kipande kifupi cha muonekano wa video hiyo ya Ni salama kutoka kwa muimbaji Eddah Mwampagama. Karibu utazame!

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Eddah Mwampagama kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 768 570 055
Facebook: Eddah Mwampagama
Instagram: @eddahmwampagama

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Fergie wa Kundi la Black Eyed Peas Aonekana Kuhudhuria Kanisani.

Next post

Serikali Ya Sweden Yawaambia Wachungaji Hawawezi Kukataa Ndoa za Jinsia Moja.