Video | Audio: Dr. Tumaini Msowoya - Nina Furaha - Gospo Media
Connect with us

Video | Audio: Dr. Tumaini Msowoya – Nina Furaha

Video

Video | Audio: Dr. Tumaini Msowoya – Nina Furaha

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam.

Mwimbaji wa muziki wa Injili pia ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Dk Tumaini Msowoya amefanikiwa kuachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa ‘Nina Furaha’.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Dk Tumaini alisema video hiyo ni ipo kwenye albamu yake ya ‘Hakuna Matata’ iliyobeba nyimbo nane.

“Ni video ya kwanza na ni nyimbo ambayo mtu akiitazama moyo wake utajaa furaha hata kama ana huzuni, ni wimbo unaompa mtu nguvu ya kusonga mbele na unaeleza wazi kwamba, mtu mwenye tumaini anayo furaha kwa sababu Mungu ndiye kiongozi wake,” alisema.

Alisema video hiyo ameifanya chini Jmic Pro chini ya Director John Gabriel huku audio ikiandaliwa na JB Production inayoongoza na Producer, Baraka Smart Billionaire.

“Ninachoomba zaidi ni saport yenu, video itakuwa kwenye Youtube Account yangu kwa hiyo, naomba muitazame na hiyo ni sapoti kubwa sana kwangu,” alisema.

Alitaja nyimbo nyingine zilizo kwenye albamu hiyo ya Hakuna Matata kuwa ni Wanawake, Mungu Mkuu, Amenitengeneza, Samehe na Mwamba.

Ni hakika utaifurahia na kubarikiwa na wimbo huu ambao nina imani kuwa utakujaza Furaha na amani kwakuwa Yesu yu ndani yako, “Nalifurahi waliponiambia na twende nyumbani mwa Bwana” – Zab 122:1.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Dr. Tumaini Msowoya kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 000 009
Facebook: Tumaini Msowoya
Instagram: @tumainimsowoya
Youtube: Tumaini Msowoya

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Video

To Top