Connect with us

Audio: Dr. Tumaini Msowoya – Hakuna Matata

Muziki

Audio: Dr. Tumaini Msowoya – Hakuna Matata

Kutoka jijini Dar es salaam, leo nimekusogezea wimbo uitwao Hakuna Matata kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Dr. Tumaini Msowoya wimbo huu umetayaarishwa na prodyuza Smart Billionea kutoka studio za Jb Production.

Akiongea na gospomedia Dr.Tumaini amesema kuwa wimbo huu ndio unaobeba jina la albamu yake mpya iitwayo Hakuna Matata ikiwa ni album yake ya pili baada ya ile ya kwanza iliyotambulika kwa jina la Natembea Kwa Imani ambayo anasema haikufanya vizuri.

Album hii yenye mkusanyiko wa nyimbo nane zenye kubariki na kutia moyo inatarajiwa kuwekwa wakfu ndani ya kanisa la KKKT iringa kuanzia saa moja asubuhi na kuzinduliwa rasmi katika ukumbi wa Highland Hall Iringa mjini siku ya jumapili ya tarehe 29.10.2017 kuanzia saa nane mchana na kuendelea.

”Hakuna Matata ndiyo wimbo unaobeba jina la albamu yangu mpya na huu ni wimbo unamuongezea mtu nguvu kwamba hata kama kuna jaribu gumu kiasi gani, kushinda ni lazima. Ukiwa na Yesu hakuna matata. . ..Kuna wakati majaribu huwa yanaumiza moyo cha msingi ni kujipa moyo. ..kutokata tamaa na kusonga mbele”. Alimaliza na kusisitiza Dr.Tumaini Msowoya na kuwasihi wakazi wote wa mkoani Iringa na mikoa ya jirani kufika siku ya uzinduzi albamu hiyo ili kumtia moyo katika kufanikisha safari yake ya kulitangaza neno la Mungu kupitia nyimbo za muziki wa Injili.

Mbali ya kuwa muimbaji wa muziki wa Injili Dr. Tumaini pia ni mtangazaji na mwandishi wa gazeti la Mwananchi, pia ni mwanaharakati wa ukombozi wa wanawake nchini Tanzania.

Kwa moyo mkunjufu gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Dr. Tumaini kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 767 000 009
Facebook: Tumaini Msowoya
Instagram: @dr.tumainimsowoya

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top