Connect with us

Download Official Music: Rehema Lupilya – Mwema

Muziki

Download Official Music: Rehema Lupilya – Mwema

Shalom mwana wa Mungu! leo tumekusogezea wimbo uitwao Mwema kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefanya vyema katika tasnia hii akifahamika kwa jina la Rehema Lupilya, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Hypersound Studios chini ya mikono ya prodyuza Oggy Keys.

Mwema ni wimbo wa kusifu uliobeba ujumbe wenye nguvu ya hamasa ya kurudisha imani na matumaini kwa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kamwe hashindwi na jambo lolote gumu kwakuwa yeye ni mfalme aliyeshinda mauti kupitia ufufuko wake na leo mtumishi wa Mungu Rehema Lupilya anatukumbusha na kutufundisha jambo kubwa la imani juu ya kumshukuru na kumtegemea Mungu katika maisha yetu ili tuweze kupokea neema na rehema zake kwakuwa yeye ni Mwema, fadhili na matendo yake hayachunguziki.

”Hata kama bado upo kwenye shida ni vyema kuendelea kuamini na kumsifu Mungu, wimbo huu ni kwa ajili ya kuwatia moyo watu walio katika shida mbalimbali na napenda kuwapa tumaini kuwa katika hali zote Mungu anaendelea kuwa mwema. Tusiache kumtumainia!! Alisema mwimbaji Rehema Lupilya.

Hakika huu ni wimbo wa kubariki sana na kuinua moyo kwa wewe mwana wa Mungu utakayebarikiwa kusikiliza wimbo na amini hautakuwa kama ulivyo baada ya kusikiliza wimbo huu uliojaa matumaini mapya hasa kwa wale wote wenye roho ya kukata tamaa kutokana na changamoto mbalimbali wanazopitia katika maisha yao.. Amini na umpokee Yesu Kristo leo ili uweze kupokea huruma yake na kubarikiwa zaidi na zaidi…

Kwa moyo wa unyenyekevu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye nguvu kukutia Moyo na kukuinua amini Mungu ni Mwema. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma za mialiko wasiliana na muimbaji Rehema Lupilya kupitia
Simu/WhatsApp: +255 719 478 315
Facebook: Rehema Lupilya
Instagram: @rehemalupilya
Email: rehemalupilya1@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top