Connect with us

Download Official Music Audio: Andrew Robinson – Ni Tayari

Muziki

Download Official Music Audio: Andrew Robinson – Ni Tayari

Kutoka jijini Mwanza leo tumekusogezea wimbo mzuri wa kuabudu uitwao Ni Tayari kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Andrew Robinson, wimbo huu ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za MP Production chini ya mikono ya prodyuza Ibrahim Ayoub.

Akiongea na timu ya habari ya gospomedia.com mwimbaji Andrew Robinson amesema: ”NI TAYARI ni wimbo unaokiri kumtumikia Mungu hata kama nipo katika mazingira magumu kiasi gani, haijalishi nilipo, ninakotoka, watu wanaonizunguka, historia ya maisha yangu, bado nakiri kuwa nitaendelea kumtumikia Mungu kwa kiwango cha juu kabisa cha Imani yangu kwake kwasababu naamini yote Mungu kupitia Bwana wetu Yesu Kristo amefanya yaliyo makuu juu yangu ili niweze kutimiza kusudi lake hapa duniani hata huduma hii aliyoianzisha ndani yangu naamini yeye ndiye atakayeniwezesha kuitenda na kuimaliza katika kiwango anachokitaka, Namuomba Mungu anigange Moyo wangu, nafsi yangu na akili zangu nisisikilize ya wanadamu juu ya huduma yangu bali nimsikilize Mungu aniongozaye, nimtukuze yeye pekee na hili ndilo kusudi kuu la wimbo huu NI TAYARI”. Alimalisema mwimbaji Andrew Robinson.

Huu ni wimbo mzuri sana wa kuabudu, kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakwenda kuwa baraka kwako na kwa wengine wote siku ya leo. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Andrew Robinson kupitia:
WhatsApp: +255 765 377 611
Facebook: Andrew Robinson
Instagram: @andrewrobinson
Email: andrewrobinson@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top