Connect with us

Download Music Audio: Peter Mdoe – Mpaji Mungu

Muziki

Download Music Audio: Peter Mdoe – Mpaji Mungu

Shalom mwana wa Mungu! leo kutoka jijini Dar es salaam tumekusogezea wimbo mpya uitwao Mpaji Mungu kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Peter Mdoe, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Republic of Music chini ya mikono ya prodyuza Mpeula.

Huu ni wimbo wa wenye nguvu kubwa ya baraka ya kukutia moyo na matumaini hasa kwa wewe mwenye roho ya kukata tamaa kutokana na mapito magumu unayopitia mwimbaji Peter Mdoe ameamua kutukumbusha tena kuwa nafasi ya Mungu katika maisha yetu ni kubwa sana tofauti na binadamu wafikiriavyo pindi tupatapo majaribu, kupitia wimbo huu mwimbaji Peter Mdoe anatusisitiza kuwa dawa ya matatizo yetu ni Mungu pekee kupitia mwanae Yesu Kristo ambaye anatupatia kibali cha ukombozi katika maisha yetu na kutengwa mbali na uovu wa shetani, hakika hii ni moja kati ya nyimbo zenye nguvu ya baraka pindi unapoisikiliza na kweli utabarikiwa.

Kwa moyo wa unyenyekevu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye baraka ya kukutia Moyo na kukuinua na endelea kuamini kuwa yote unayopitia ipo siku yatakwisha kwakuwa Mpaji ni Mungu tu. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Peter Mdoe kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 655 094 891
Facebook: Peter Mdoe
Instagram: @peter_mdoe

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top