Connect with us

Download Music Audio: New Jerusalem Feat Neema Busee – Mary Did You Know

Audio

Download Music Audio: New Jerusalem Feat Neema Busee – Mary Did You Know

Kutoka jijini Dar es salaam leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tunakaribisha kusikiliza wimbo mpya kutoka kundi la vijana wenye uwezo mkubwa wa kutumia sauti na kukamilisha wimbo bila kutumia vyombo vya muziki na hawa si wengine bali ni New Jerusalem Brothers, wimbo huu unaitwa Mary Did You Know wakiwa wamemshirikisha mwanadada anayefahamika kwa jina la Neema Busee, wimbo ukiwa umeandaliwa na producer Vankuva kutoka studio ya HomeTown iliyopo Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com mmoja wa kiongozi wa kundi hilo la Bw.Clinton Onditi amesema kuwa wanamshukuru Mungu kwa mara nyingine kwa kuikamilisha kazi hii ambayo wanaamini itakwenda kumgusa kila mtu kwa namna yake na itakuwa baraka tena kwa wapendwa wote hasa wale wanaofutilia kazi na huduma zao kutoka ndani na nje ya Tanzania, Hata hivyo amesisitiza kuwa kwasasa wapo kwenye maandilizi ya kukamilisha album yao ambayo wataizindua na kuachia sokoni muda w0w0te kuanzia sasa.

Kundi hili la New Jerusalem Brothers limeundwa na vijana sita ambao ni Clinton Onditi, Francis bisanda, Elia Mchomvu, Erasto Chacha, Jacob Silas na Bulongo Masatu.

gospomedia.com inakukaribisha kuusikiliza na kupakua wimbo huu kutoka kundi la New Jerusalem Brothers na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na kundi la New Jerusalem Brothers kupitia:
Simu/WhatsApp: +255757830451 au +255657184087
Facebook: New J Brothers
Instagram: newjerusalembrotherstz
YouTube: Officialnewjerusalembrotherstz
Email: newjerusalebrotherstz@gmail.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram > @gospomedia

More in Audio

To Top