Audio

Download Music Audio: Love Mdendu – Chozi la Mnyonge

Kutoka jijini Arusha Tanzania blog ya gospomedia.com leo inamtambulisha kwako mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Love Mdendu wimbo huu unaitwa Chozi la Mnyonge ukiwa ni wimbo ulioandaliwa na kutengenezwa ndani ya studio za Habari Maalum chini ya usimamizi wa kampuni ya Genecic iliyopo jijini Arusha.

Love Mdendu ni mwimbaji wa nyimbo za Injili aliyezaliwa katika familia ya kitumishi na alianza kuimba tangu akiwa Sunday school katika kanisa alilokuwa anachunga baba yake. Baadae alijiunga na kwaya ya kanisa na kuhudumu kwa muda na sasa ameamua kufanya kazi zake binafsi chini ya usimamizi wa kampuni ya Genecic promotions ambayo ndio imesimamia kurekodiwa kwa wimbo huu katika studio za Habari maalum.

Blog ya gospomedia.com inakukaribisha kwa moyo mkunjufu kusikiliza na kupakua wimbo huu wa Chozi la Mnyonge kutoka kwa mumbaji Love Mdendu, usiache kuwashirikisha na wengine wimbo huu kwa kadri uwezavyo ili Injili iweze kuwafikia watu wengi zaidi mahali pote duniani na hakika utabarikiwa sanaKaribu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Love Mdendu kupitia
Simu/WhatsApp: +255 656 450 681
Facebook Page: Genecic
Instagram: @genecicpromotions
Youtube: Genecic promotions

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mafanikio: Fahamu Jinsi ya Kufanikiwa - Sehemu ya Pili

Next post

Download Official Music Audio: Elvis Kiwanga - The Word (Neno)