Audio

Download Music Audio: God Surrender Feat Jenipher Sitta-Uweponi

Shalom! kutoka Arusha Tanzania tovuti ya gospomedia.com leo inakuletea wimbo mpya unaoitwa Uweponi kutoka kwa kwa mwana gospel HipHop anayefahamika kwa jina la God Surrender akiwa amemshirikisha mwanadada Jenipher Sitta, wimbo ukiwa umetengenzwa na producer Justinoo kutoka Arusha.

God Surrender ameongea na gospomedia.com na hiki ndicho alichosema “Napenda kumshukuru Mungu kwa kuruhusu nizaliwe katika dunia nzuri na yenye kupendeza, wapo wengi tuliozaliwa nao Siku moja lakini leo hawapo, lakini mimi amenipa neema ya kuwa hai na ninaishi kwa upendeleo wake, zaidi sana amenipa kipawa cha kumtumikia, napenda NIKAE UWEPONI maisha yangu yote nizidi kumjua na kumfahamu”….. tarehe 31.10.2016 ni Siku ya kukumbuka kuzaliwa kwangu na Siku hii nimeona niisherekee na kuifurahia kwa kumshukuru MUNGU pamoja na marafiki, ndugu na jamaa zangu wa karibu…ambapo siku hii nimeona vyema kuachia nyimbo yangu mpya iitwayo UWEPONI MWAKO…… Uweponi Mwako ni nyimbo inayoyagusa maisha yangu baada ya miaka kadhaa iliyopita nilipokua mtoto wa mitaani (street children) ambapo niliishi maisha ya utumwani, maisha ya huzuni na mateso ambapo nililala mitaroni na kula mabaki ya vyakula vilivyotupwa majalalani, na kushiriki matendo mabaya yasiyompendeza MUNGU…Leo hii nimeokoka nimefanywa MTU mpya na kwa kutambua ni Yesu aliyeniokoa ndio maana nataka NIKAE UWEPONI …nikae na MUNGU, niishi na yeye, maisha yangu nimeyatoa kwake yeye aniongoze….NIKAE UWEPONI ni nyimbo yangu ya pili baada ya kuachia The Way U are….”

gospomedia.com tunakukaribisha kuupakua(kudownload) na kuusikiliza wimbo huu wa Uweponi kisha uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kumpa sapoti mwana gospel hiphop huyu God Surrender na wengine waweze kubarikiwa pia kupitia wimbo huu na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!!

DOWNLOAD

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na God Surrender wasiliana nae kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 767 650 266
Facebook: God Surrender’s Tz
Instagram: @godsurrender
Email: surrender4g@gmail.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram > @gospomedia

 

Advertisements
Previous post

Pure Mission Wanakuletea Huru Festival ndani ya Iringa,Usiku wa Novemba 4.Fahamu zaidi hapa.

Next post

Xclusive Chat with Kraist Kid: Kuhusu kuchaguliwa kwenye kwenye tuzo za Xtreem na Jinsi ya kumpigia kura.