Download Music Audio: Gideon Mussa-Africa - Gospo Media
Connect with us

Download Music Audio: Gideon Mussa-Africa

Audio

Download Music Audio: Gideon Mussa-Africa

Shalom!! Kutoka nairobi kenya, leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tunautambulisha kwako wimbo mpya kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Gideon Mussa wimbo unaitwa Africa ukiwa umetengenezwa na producer Daggie kutoka Step Studio Nairobi.

Akiongea na GospoMedia.com Gideon Mussa amesema kuwa wimbo huu wa Africa ni wimbo unaobeba jina album yake mpya ambayo ipo kwenye mfumo wa Audio CD na DVD ambayo ilizinduliwa tarehe 29.09.2016 uwanja wa CCM Kirumba ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo saba na video saba na tayari zimeshakamilika na sasa yupo kwenye taratibu za kukamilisha usambazaji wa album hiyo na atatoa taarifa pindi album hiyo itakapoingia sokoni.

gideon2

Album mpya ya mwimbaji Gideon Mussa inayoitwa AFRICA iliyo kwenye mfumo wa Audio CD na DVD.

Gideon Mussa ameongeza kuwa album hii mpya ya Africa ina mkusanyiko wa nyimbo zenye baraka na za kuwainua watu zaidi katika kuwakumbusha juu ya kumtumikia Mungu katika roho na kweli na kufanya yanayompendeza yeye kwa matendo matakatifu.

Kupitia nyimbo zilizo kwenye abum hii ya Africa anaamini zitawatakasa zaidi watu wengi kila watakapokuwa wanazisikiliza nyimbo na kuangalia video zake pia, hivyo amewataka wadau na mashabiki wake wote kutoka Afrika mashariki na pande zote za dunia kumuunga mkono kwa kuinunua album yake hii mpya ya Afrika pindi itakapoingia sokoni.

gospomedia.com tumekuwekea wimbo huu wa Afrika uweze kuupakua(kuudownload) na kuusikiliza kisha uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili wengine pia wapate kubarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu wa Afika kutoka kwa mwimbaji Gideon Mussa. Karibu!!

DOWNLOAD

Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kuipata nakala ya album yake mpya na huduma za mialiko wasiliana na mwimbaji Gideon Mussa kupitia
Simu/WhatsApp: +254 725 942647
Facebook: Gideon Mussa
Instagram: @gideonmussa
E-mail: gideonmussa82@gmail.com

Youtube: Gideon Mussa

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Continue Reading
You may also like...

More in Audio

To Top