Connect with us

Download Music Audio: Gelax Wakristo Feat. Henry Ngosi – King’ora

Muziki

Download Music Audio: Gelax Wakristo Feat. Henry Ngosi – King’ora

Kutoka kwenye album yake  mpya iitwayo Wakristo EP Volume 1, Rapa Gelax Wakristo anakukaribisha tena kusikiliza wimbo wake wa tatu kutoka kwenye albamu hiyo, wimbo huu unaitwa King’ora akiwa amemshirikisha Henry Kingosi ukiwa umetaayarishwa na Prodyuza Amzy kutoka studio ya Enzi Records iliyopo jijini Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia rapa Gelax amesema kuwa King’ora ni wimbo unaoelezea Injili kwa mfano wa Kin’gora, kama jinsi ilivyo maana yake King’ora inaashiria hali ya hatari au tukio fulani ambalo sio zuri lililotokea katika jamii na kuwasihi watu kuwa waangalifu.

” Nimezungumzia Ving’ora vya aina mbili, katika beti(verse) ya kwanza nimezungumzia king’ora cha polisi ambacho mara nyingi kikisikika mtaani kinafanya wanaofanya uhalifu kuacha na kukimbia kujificha, ndivyo Injili inavyokuja kwa wote wanaotumikishwa na dhambi, inakuja kuwakoa wao pia kuleta usalama kwenye mtaa na jamii kwa ujumla, Kwa hiyo Injili ikilia mtaani kazi za shetani uhalifu, uovu unaharibiwa. Katika beti (verse) ya pili nimezungumzia King’ora cha ambulance ambacho mara nyingi kinapolia sehemu yoyote au kama ni ajali imetokea yule aliyepata ajali akisikia King’ora anasikia kupata uzima kwakuwa huduma ya kuponywa kwake inakuwa imefika, Kadhalika Injili inapokuja kwa wagonjwa wa rohoni wanapata kupona kabisa na kuachana na yale maovu yao, kama ni ajali wadhani ni kawaida kumbe huwa ni mipango ya shetani pia, hivyo hii ni Injili kupitia picha ya King’ora. ” Alisema Gelax Wakristo.

Gelax ameongeza kwamba tayari album hii ya Wakristo (EP) Volume 01 imeshaingia mtaani rasmi na inapatikana kwa kiasi cha shilingi elfu 3,000/ tu za kitanzania, Hivyo amewataka wapenzi na wadau mbalimbali wa muziki wa Injili kumuunga mkono kupitia albamu yake hiyo ambayo ameinadi kuwa ni ya kipekee sana, ikiwa imekusanya nyimbo zenye jumbe zenye baraka na zenye kuinua sana moyo hivyo watu wote wasikose kuitafuta na kuipata.

Kwa moyo mkunjufu gospomedia.com tunakukaribisha kuusikiliza na kuupakua wimbo huu ambao tunahakika utakubariki sana, pia washirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo na katika kumpa sapoti usiache kuinunua album hii ambayo pia itakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi juu ya kuipata nakala ya album yake ya Wakristo (EP) Volume 01 au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Gelax Wakristo kupitia
Simu/WhatsApp: +255 657 140 440
Facebook: Gelax Wa Kristo
Instagram: @gelaxwakristo
Twitter: @gelaxwakristo

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Continue Reading
Advertisement
You may also like...
Advertisement

TRENDING

To Top