Connect with us

Download Music Audio: Dr.Tumaini Msowoya – Furaha

Muziki

Download Music Audio: Dr.Tumaini Msowoya – Furaha

Kutoka jijini Dar es salaam, leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekusogezea wimbo mpya uitwao Furaha kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Dr. Tumaini Msowoya wimbo ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Smart Billionea kutoka studio ya Jb Production.

Akiongea na gospomedia Dr.Tumaini amesema kuwa wimbo huu wa Furaha utapatikana kwenye album mpya iitwayo Hakuna Matata ikiwa ni album ya pili baada ya ile ya kwanza iliyotambulika kwa jina la Natembea Kwa Imani ambayo haikufanya vizuri.

Album hii yenye mkusanyiko wa nyimbo nane  zenye kubariki na kutia moyo inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 29.10.2017 katika kanisa la KKKT Iringa Mjini, baada ya kuwekwa wakfu jijini Dar es salaam.

Katika wimbo huu Dr.Tumaini amezungumzia juu ya Furaha ya kweli inayopatikana ndani ya mtu mara baada ya kukabidhi maisha yake kwa Yesu Kristo na kusisitiza kuwa hakuna amani ya kweli inayopatikana katika maisha ya mtu hapa duniani kama hajaamua kukabidhi maisha yake kwa Yesu Kristo kwakuwa yeye ndiye ndiye mwanzo na mwisho katika kutetea na kuokoa maisha yetu kila siku.

Mbali ya kuwa muimbaji wa muziki wa Injili Dr. Tumaini pia ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi, pia ni mwanaharakati wa ukombozi wa wanawake nchini Tanzania.

Kwa moyo mkunjufu gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao hakika utakubariki sana na kukufanya uwe na Furaha kila utakapokuwa unausikiliza. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Dr. Tumaini kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 767 000 009
Facebook: Tumaini Msowoya
Instagram: @dr.tumainimsowoya

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top