Audio

Download Gospel Music Audio: Samwel Gospel – Fungua Maisha Yangu

Kutoka Jjijini Dar es salaam Tanzania, tovuti yako pendwa ya gospomedia.com leo inautambulisha kwako wimbo mpya uitwao Fungua Maisha Yangu kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Samwel Gospel wimbo ukiwa umetengenzwa chini ya mikono ya maproducer wawili ambao ni Paul na 1 Touch.

Muimbaji Samwel Gospel ameanza kuimba mwaka 2014 na kuingia studio rasmi mwaka 2015 na kuanza kurekodi kazi zake na hatimaye wimbo wa Fungua Maisha yangu ulifanikiwa kurekodiwa mwaka 2016. Kupitia safari yake ya muziki muimbaji Samwel Gospel amepitia changamoto nyingi, ikiwemo kutopata nafasi anapoingia studio na kuwekwa foleni kwa muda mrefu sababu kubwa ni uhaba wa pesa.

Kuhusu Malengo muimbaji Samwel Gospel amesema kuwa lengo lake kubwa ni kusukuma Injili na huduma yake ya uimbaji iweze kuwafikia watu wengi zaidi kwa njia ya muziki wa Injili ambao ndio wito wangu kwa Mungu kwa kulitangaza jina lake na watu waweze kupona kupitia huduma hii. na wito wake kwa wataarishaji wa muziki (producers na video directors) Muimbaji Samwel Gospel amewaomba wafanye kazi kwa kiwango kikubwa kwa waimbaji wote na waache matabaka maana hawajui wanaomuona leo ni mchanga hawajui kesho atakuwa muimbaji mkubwa hivyo wanavyowafanyia waimbaji waliotangulia hivyo hivyo na waimbaji wanaoanza wapewa uthamani kama wale waliotangulia kwenye muziki huu pia na kwa waimbaji wanaoanza muziki wasikate Tamaa katika kufanya huduma hii  kwakuwa Mungu atawainua kikubwa ni kumtanguliza Mungu Mbele.

gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wa Fungua Maisha Yangu kutoka kwa mumbaji Samwel Gospel na uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo  ili nao waweze kubarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu na hakika Mungu atakubariki sana.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Samwel Gospel kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 652 633 171
Facebook: : Samwel Gspel
Instagram: @samwelgspel
YouTube: Samwel Gspel

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Gospel Music Audio: Joel Milendo Feat Mussa Mpume - Mtetezi

Next post

Fahamu Jinsi Ya Kufanikiwa: Sehemu ya Kwanza