Audio

Download Gospel Music Audio: Joel Milendo Feat Mussa Mpume – Mtetezi

Kutoka mjini Dodoma Tanzania, tovuti yako pendwa ya gospomedia.com leo inautambulisha kwako wimbo mpya uitwao Mtetezi kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Joel Milendo akiwa amemshirikisha Mussa Mpume wimbo ukiwa umetengenzwa ndani ya studio ya Adonai Records chini ya mikono ya Producer Danny kutoka jijini Mwanza.

Akiongea na timu habari ya gospomedia muimbaji Joel Milendo amesema kuwa “wimbo wa Mtetezi ni wimbo ambao unabeba ujumbe mzito wa Mungu katika maisha yetu kama Mtetezi wetu.. Uumbaji wetu kwa jinsi ya mwilini unaweza usielewe ni mangapi Mungu ameyaepusha dhidi yako na ni vita gani Mungu ana pigana kwa ajili yako haijalishi unawafahamu Maadui zako au lah!! Lakini kama alivyo mtetea Daudi dhidi ya mishale ya  Sauli (samweli 18:11,12) ndivyo amefanya imara ulinzi kwaajili yetu dhidi ya maadui zetu hata tunaendelea kuishi.. Hivyo  tunakila sababu ya kumtukuza Mungu haijalishi tunapitia changamoto gani , tukiamini tu kuwa mtetezi wetu  yupo hai na tutaenda kumuona akijiinua katika  hayo sawa na Ayubu 19:25.. Mungu Awabariki sana!!!

gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu wa Karibu Nyumbani kutoka kwa mumbaji Joel Milendo na uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo  ili nao waweze kubarikiwa na kuinuliwa kupitia wimbo huu na hakika Mungu atakubariki sana.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Joel Milendo kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 719 566 792
Facebook: : Joel Charls
Instagram: @milendojoel
YouTube: Joel Milendo
Email: joelmilendo@gmail.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Download Music Audio: Jeremiah Masasi - Karibu Nyumbani

Next post

Download Gospel Music Audio: Samwel Gospel - Fungua Maisha Yangu