Download Gospel Music Audio: Edwin Mrope - Piga Kelele - Gospo Media
Connect with us

Download Gospel Music Audio: Edwin Mrope – Piga Kelele

Audio

Download Gospel Music Audio: Edwin Mrope – Piga Kelele

Kutoka jijini Dar es Salaam Tanzania tovuti ya gospomedia.com leo inautambulisha kwako wimbo mpya uitwao Piga Kelele wenye mahadhi ya singeli kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Edwin Mrope wimbo ukiwa umetengenezwa ndani ya studio ya Edwin Mrope chini ya mikono yake mwenyewe akiwa kama producer wa studio hiyo iliyopo hapa jijini Dar es salaam.

Akiongea na timu ya gospomedia.com Muimbaji Edwin Mrope amesema kuwa wimbo huu unaitwa Piga Kelele kama vile Zaburi 150 inavyotuagiza kumsifu MUNGU kwa njia mbalimbali. Wimbo huu pia unahimiza kumsifu MUNGU bila kujali vyeo vyetu na ustaarabu wetu kwa kuwa Yeye ni Mkuu sana. Kuhusu mahadhi ya singeli yaliyotumika katika wimbo huu Edwin Mrope amesema kuwa ameona atumie mahadhi hayo ya singeli kwasababu anaamini ni style(mtindo) ya asili ya muziki wa kitanzania.

gospomedia.com tunakupa nafasi ya kusikiliza na kupakua wimbo huu wa Piga Kelele kutoka kwa muimbaji Edwin Mrope na uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili waweze kubarikiwa na kuisaidia Injili kusambaa kwa watu wote na hakika Mungu atakubariki sanaKaribu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma na jinsi ya kuipata album wasiliana na mwimbaji Edwin Mrope kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 246 084
Facebook: Edwin Mrope
Instagram: @Edwin Mrope

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

More in Audio

To Top