Connect with us

Download Audio: Rungu la Yesu – Uandishi na Flow

Muziki

Download Audio: Rungu la Yesu – Uandishi na Flow

Shalom Shalom mwana wa Mungu!! leo ni siku nyingine ya kupokea baraka kutoka kwa rapa mahiri na mkongwe katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania huyu si mwingine bali ni Rungu la Yesu ambaye leo amekusogezea rasmi wimbo wake mpya uitwao ”Uandishi na Flow” ukiwa umetaayarishwa ndani ya studio ya House Of Music chini ya mikono ya prodyuza anayefahamika kwa jina la Makharythm kutoka jijini Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com rapa Rungu la Yesu amesema haya kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu “Maana halisi ya wimbo huu wa ”Uandishi na Flow” ni kuandika na kuimba ulichokiandika, kusema kile unachokiamini iwe kukipenda au kutokipenda au kwa kuonya au kufundisha bila kuficha wala kupindisha pindisha maneno. Huu ni wimbo flani ambao mimi kama Rungu la Yesu nimeamua kuzungumzia mambo mengi kama vile, wanaume kupiga wake zao kisa eti ushabiki wa timu au vyama, vita ya sisi na umasikini itaisha tu pale siku tunaingia kaburini, mtaani kwa sasa hakuna ajira watu ni wezi na mabinti wamekuwa malaya, kingine nimezungumzia watu kuacha lawama, badala ya kumlaumu raisi basi tutumie muda huo kumwombea kwa MUNGU maana MUNGU ni mkuu kuliko raisi ambaye akimgusa raisi maombi yenu yanajibiwa.. nimeendelea kusema kwamba taarifa mbaya kwa watoto wa MUNGU zote nikuzifuta kwa NENO na DAMU ya YESU…nimesisitiza pia waimbaji wa Injili WAIMBE Injili ili MUNGU atukuzwe..sikuacha kusema unapotaka MUNGU akupende basi na wewe uwe tayari kuonyesha upendo kwa MUNGU na kwa jamii pia…Mwisho nimewaasa watu kumtegemea MUNGU na kumwabudu siku zote hata kama mambo yatakuwa magumu vipi tusimfungulie mlango shetani kivyovyote vile……” alimaliza Rungu.

Kwa moyo mkunjufu kabisa kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao tunahakika utakwenda kukubariki na kukuinua kutokana na ujumbe mzito uliojaa katika wimbo huu ”Uandishi na Flow” Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Rungu La Yesu kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 348 032 au +255 752 777 721
Facebook: Rungu L a Yesu
Instagram: @rungulayesu
Email: rungulayesu@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Continue Reading
Advertisement
You may also like...
Advertisement

TRENDING

To Top