Download Audio: Rogate Kalengo - Ibada - Gospo Media
Connect with us

Download Audio: Rogate Kalengo – Ibada

Audio

Download Audio: Rogate Kalengo – Ibada

Kutoka jijini Dar es salaam leo kupitia blog yako pendwa tumesogezea wimbo mpya kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Tanzania ambaye alikuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya Gospel Star Search mwaka 2016 huyu si mwingine la Rogate Kalengo wimbo huu unaitwa Ibada ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio ya Faith Music Lab (Fm Studio) chini ya mikono ya producer Modern music & Mr.Forever anayepatikana jijini Dar es salaam.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Rogate Kalengo alikuwa na haya ya kusema juu ya wimbo huu ”Nilikuja kugundua kuwa kuimba kwa sauti kuu, kwa vinanda na filimbi na kila aina ya ala za muziki katika ubora wake zinaweza kuwa kelele kwa MUNGU kama mioyo yenu ipo mbali naye. Ni Muhimu kuitoa miili yenu iwe dhabihu safi kwa maana hiyo ndiyo IBADA yetu yenye Maana. unapousikiliza wimbo huu hilo liwe ombi lako, WARUMI 12:1” Alimaliza Rogate Kalengo.

Mashairi ya wimbo IBADA:

Natoa Ibada
kutoka ndani
ya moyo wangu
moyo wangu

IBADA
IBADA
IBADA
ya Moyo wangu

mimi ni nani bila wewe
hata niishi bila wewe
maana siwezi bila wewe
na nitapotea bila wewe
wewe ni jana yangu Bwana
wewe ni leo yangu Bwana
wewe ni kesho yangu Bwana
wewe ni milele yangu Bwana
nami naishi kukwabudu
mikono yangu nainua
na mwili wangu uwe dhabihu
uwe IBADA

Nakuabudu Bwana
nakuinua Bwana
wewe ni MUngu wangu
Mfalme

oouooh
oouooh
Hii ni Ibada
ya Moyo wangu.

 

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kuupakua wimbo huu na hakika utafanyika Ibada katika maisha yako. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Rogate Kalengo kupitia
Simu/WhatsApp: +255 752 254 801 au +255769103087
Facebook: Rogate Kalengo
Instagram: @rogatekalengo
YouTube: Rogate Kalengo
Email: rogatekalengo@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

More in Audio

To Top