Connect with us

Download Audio Music: Judith Mbilinyi – Maisha Yangu

Muziki

Download Audio Music: Judith Mbilinyi – Maisha Yangu

Bwana Yesu Asifiwe! leo kwa uwezo wa Mungu nimekusogezea wimbo wenye baraka nyingi sana uitwao Maisha Yangu kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za kuabudu kutoka jijini Dar es salaam Tanzania anayefahamika kwa jina la Judith Mbilinyi. Wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za EM Records chini ya mikono ya prodyuza Erasto Augustino.

Hii ni moja kati ya nyimbo zenye mafuta ya pekee sana ya upako katika kumwabudu Mungu ambaye kupitia Bwana wetu Yesu Kristo ameachilia nguvu kwa mtumishi Judith Mbilinyi ambaye kupitia wimbo huu ameonekana kuwa katika uwepo wa kipekee wa Mungu akilisifu jina la Yesu Kristo na kuzikumbusha nafsi zetu pia kuwa maisha yetu yapo mikononi mwa Bwana wete Yesu na huu ni ujumbe wake maalumu aliutoa kuhusu wimbo huu kwetu;

”Ashukuriwe Yesu alieachilia neema na kibali cha kuuhifadhi wimbo huu katika sauti (audio), ninatamka ushindi, kuinuliwa, kuhuishwa, kuponywa kupitia wimbo huu, unapousikiliza basi nguvu ya Mungu ikutembelee hapo ulipo in Jesus name. Zaburi 143:10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako, Kwa maana ndiwe Mungu wangu; Roho yako mwema aniongoze kwenye nchi sawa.”

Kwa moyo wa unyenyekevu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao nina hakika utakwenda kukubariki katika viwango vingine vya kumwabudu na kumsifu Mungu. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Judith Mbilinyi kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 762 372 408
Facebook: Judith Mbilinyi
Instagram: @judithmbilinyi
Youtube: Judith Mbilinyi

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

NAWAPENDA - ZABRON SINGERS

Muziki

VIDEO | NAWAPENDA – ZABRON SINGERS

By October 11, 2021

TRENDING

To Top