Connect with us

Download Audio Music: Gilbert Noah – Usiniache

Muziki

Download Audio Music: Gilbert Noah – Usiniache

Bwana Yesu asifiwe!! leo kwa utukufu wa Mungu nimekuwekea wimbo mzuri uitwao Usiniache kutoka kwa mwimbaji na mtaayarishaji wa nyimbo za Injili Gilbert Noah kutoka jijini Mwanza, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Exodus chini ya mikono yake mwenyewe.

Usiniache ni wimbo wa sifa na unyenyekevu mbele za Mungu ukizungumzia wema na upendo wa Bwana wetu Yesu ambao ndio chanzo cha uhai wetu, furaha yetu, amani na hata mafanikio yetu na sasa kupitia wimbo huu tunakiri kuwa yeye ndiye Bwana na mwokozi wa maisha yetu na kwa unyenyekevu mkubwa mwimbaji Gilbert Noah anatukumbusha kuwa ili tuweze kupokea baraka na kuwa mbali na mikono ya shetani ni lazima tutengeneze mahusiano mazuri na Mungu ili kutupatia ulinzi imara kupitia Roho wake mtakatifu. Huu ni wimbo wa kubariki sana ukiwa ukiwa na mpangilio mzuri wa vyombo vya muziki na uimbaji utakaokufanya kutamani kusikiliza mara kwa mara na hakika utapata kumtukuza Mungu katika kiwango cha juu kupitia wimbo huu.

Akiongea na gospomedia.com mwimbaji Gilbet Noah amesema kuwa wimbo huu utapatikana kwenye album yake mpya atakayoiachia mwishoni mwa mwaka huu wa 2017 hivyo amewasihi wadau na watu wote wanaopenda muziki wa Injili kuwa wavumilivu ili waweze kuipokea albamu hiyo ambayo amesema itakuwa ni yenye mkusanyiko wa nyimbo zenye kubariki na kuinua sana.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakwenda kubadilisha maisha yako siku ya leo. Karibu tumsifu Mungu.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Gilbert Noah kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 759 509 779
Facebook: Gilbert Noah
Instagram: @noahgilbert15
Email: noahgilbert15@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

GUARDIAN ANGEL - NI TABIBU_audio

Muziki

AUDIO | GUARDIAN ANGEL – NI TABIBU

By September 22, 2021

TRENDING

To Top